Watendaji waliosababisha wanafunzi hewa kuchukuliwa hatua za kinidhamu

Na. Fred Kibano

Watendaji waliosababisha wanafunzi hewa kuchukuliwa hatua za kinidhamu

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhe. George Simbachawene (MB) amewaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa kuchukua hatua za kinidhamu juu ya wote waliohusika kufanya udanganyifu wa kitakwimu na kuzalisha wanafunzi hewa kwa lengo la kuongeza kiwango cha fedha za matumizi ya Serikali mashuleni.

Alisema kutokana na zoezi la uhakiki waliloliendesha idadi ya wanafunzi hewa ni 65,198 kwa shule za msingi na sekondari na kama wasingebainika kiasi cha shilingi 931,317,500 katika mwaka wa fedha 2016/2017 zingepelekwa na kupotea kwa kuwahudumia wanafunzi hewa.

Akiongea na waandishi wa habari ofisini kwake mjini Dodoma Mhe. George Simbachawene (MB) ambaye pia ni Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa amesema zoezi la uhakiki wa wanafunzi hewa kwa shule za Msingi na Sekondari nchini limefanikiwa kwa kiasi kikubwa tangu kutolewa kwa agizo la Mhe. Rais John Pombe Magufuli mnamo mwezi Agosti mwaka huu.

Amesema baada ya zoezi la uhakiki hadi kufikia mwezi Septemba, 2016 kwa kutumia madodoso ya Shule za Awali, Takwimu za shule za Msingi, Takwimu za Shule za Sekondari na nyaraka za mahudhurio ya wanafunzi jumla ya wanafunzi hewa kwa shule za Msingi ni 52,783 na 12,415 kwa shule za Sekondari na idadi yao jumla ikiwa ni 65,198.

Mkoa unaoongoza kwa kuwa na wanafunzi hewa ni Tabora wanafunzi 12,112, Ruvuma 7,743, Mwanza 7,349 na mingineyo ambayo taarifa yake inapatikana katika mtandao wa OR TAMISEMI (www.tamisemi.go.tz).

"hatua za kinidhamu zitachukuliwa kwa wale wote waliosababisha uwepo wa wanafunzi hewa, aidha Ofisi ya Rais TAMISEMI inaendelea kuhakiki takwimu zilizowasilishwa," alisisitiza Mhe. Simbachawene.

Aidha, amewaagiza viongozi katika mikoa Tanzania Bara kuhakikisha kutokuwepo tena kwa wanafunzi hewa katika mikoa yao kwani Serikali haitegemei haitasita kuchukua hatua pale inapostahili. "Nawaagiza Makatibu Tawala wa Mikoa, Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa na Wakuu wa shule hakikisheni suala la wanafunzi hewa halijitokezi tena katika shule zote za Msingi na Sekondari."

Awali kabla ya uhakiki mwezi machi mwaka huu idadi ya wanafunzi katika shule za msingi ilikuwa ni 9,746,534 na kwa upande wa sekondari ilikuwa ni 1,483,872 ambapo baada ya uhakiki wanafunzi halali ni 9,690,038 kwa shule za msingi na wanafunzi 1,429,314 kwa sekondari.

Mapema baada ya kuingia madarakani Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania alitoa maelekezo kwa Viongozi wakiwemo Mawaziri, Wakuu wa mikoa, Makatibu Tawala wa Mikoa kuhakiki watumishi hewa na Wanafunzi hewa lakini suala la wanafunzi hewa limekwisha kamilika.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.