Waziri ataka Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa ibuni vyanzo vipya vya fedha

Na Nasra Mwangamilo

Waziri ataka Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa ibuni vyanzo vipya vya fedha

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Mh. George Simbachawene ameitaka Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa kuziongezea serikali za mitaa fursa ya kupata fedha za kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi hasa katika miradi ya maendeleo na utoaji wa huduma za kijamii.

Waziri Simbachawene ameyasema hayo mara baada ya kukutana na wajumbe wapya wa Bodi ya Mikopo ya Serikali za Mitaa katika mkutano uliofanyika mjini Dodoma ambapo alidai kuwa kitendo cha Bodi hiyo kupokea maombi yanayofikia bilioni 49 huku Bodi hiyo ikifanikiwa kutoa mikopo yenye thamani ya shilingi bilioni tisa tu.

"Natambua kuwa nyenzo muhimu za kutekeleza majukumu ya bodi ni rasilimali fedha ambazo zinatakiwa zipatikane kupitia vyanzo mbalimbali ambavyo vimeainishwa kwa mujibu wa sheria, kifungu cha 62 cha sheria ya bodi ya mikopo kinataja njia mbalimbali ikiwemo kupata fedha kama zitavyoainishwa na bunge kwa madhumuni ya kuendesha shughuli za bodi," alisema Mh. Simbachawene.

Aidha waziri alisisitiza kuwa Bodi mpya ijitahidi kusimamia kwa ukaribu zaidi uwekezaji kwa kuelekeza rasilimali kwenye vitega uchumi vyenye faida kubwa ikiwa ni njia mojawapo ya kujiongezea mapato matarajio yakiwa ni kuhakikisha bodi inatoa mikopo kulingana na makubaliano baina ya Bodi na halmashauri husika.

Pia aliwataka wajumbe wa bodi kusimamia kwa ukaribu utendaji wa bodi hiyo na kuhakikisha kwamba hesabu zinatunzwa vizuri na taarifa zinatolewa kwa wakati hii ni pamoja na kuweka amana za muda maaalumu kwenye mabenki, umiliki wa hisa katika mabenki, kodi ya pango kutoka kwenye nyumba zinazomilikiwa na bodi pamoja na malipo ya riba kutoka kwenye mikopo inayotolewa na bodi.

"Nitumie nafasi hii kusisitiza kwamba wajumbe wa bodi hii lazima kusimamia kwa ukaribu utendaji wa bodi ya mikopo na kuhakikisha kwamba hesabu zinatunzwa vizuri, ni vizuri taarifa za bodi zipatikane kwa wakati na kuwasilishwa mbele ya bodi na kujadiliwa kwa wakati," alisisitiza Waziri.

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.