• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu

Wataalamu wa Mipango wapigwa msasa, Maandalizi ya Bajeti 2019/20

Imewekwa tar.: December 14th, 2018

Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia masuala ya Afya Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Dk. Zainabu Chaula amewataka Makatibu Tawala Wasaidizi wa Mikoa Sehemu ya Mipango na Uratibu sambamba na Maafisa Mipango wote wa Halmashauri nchini kutumia taaluma zao katika kukuza uchumi wa nchi ili kuleta matokeo chanya kwa jamii.

Dk, Chaula ameyasema hayo wakati  wa Ufunguzi wa Mafunzo ya Maandalizi ya Mipango na Bajeti katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa mwaka wa Fedha 2019/20 yanayofanyika kwa siku mbili Jijini Dodoma katika ukumbi wa Mikutano wa Royal Vilage Hoteli.

Dk. Chaula amesema mafunzo hayo ni fursa kwa maafisa hao kuhakikisha wanapata ujuzi na uelewa zaidi wa namna sahihi ya uandaaji wa Mipango na Bajeti katika Mikoa na Halmashauri.

“Ili kufikia matokeo bora ya kukuza uchumi wa nchi hii mnatakiwa kuwa wabunifu na kuhakikisha  mnabadilisha changamoto kuwa fursa kitu ambacho kitabadili dhana iliyopo kwa sasa kwa wananchi kulalamikia changamoto hizo na badala yake wazitumie kuwa fursa za kuwaletea maendeleo ” Alisema Dk. Chaula.

Aliongeza kuwa sisi wataalamu tupo hapa kwa niaba  ya wananchi hivyo tunatakiwa kuleta mipango itakayowezesha wananchi hao kujikwamua kiuchumi na kujiletea maendeleo endelevu na hili litafikiwa endepo mipango na bajeti inakwenda sambamba na fursa zinazopatikana katika maeneo yetu.

Aidha Dk. Chaula ameongeza kuwa kila mtumishi wa Umma anadhamana kubwa kwa taifa  na dhamana yenyewe ni kuhakikisha tunawatumikia vyema watanzania wenzetu ili kuleta matokeo bora kwa nchi yetu kama Muhasisi wa Taifa hili Mwalimu Julius Kambarage Nyerere alivyo fanya na mpaka leo kupitia matokeo yake tunamkumbuka.

Aidha Mkurugenzi wa Idara ya Sera na Mipango OR-TAMISEMI Bw. John Cheyo, amesema kuwa kupitia mafunzo hayo maafisa hao watapata  uelewa aidi ya namna ya kuandaa bajeti iliyobora na halisi na zaidi watakuwa walimu wazuri kwa maafisa wengine katika maeneo yao ya kazi ambao hawajabahatika kupata mafunzo haya.

Naye Mkurugenzi wa Mradi wa Uimarishaji Mifumo ya Sekta ya Umma (PS3), Dk. Emanuel Malangalila amewataka  kuwa maafisa waliopata mafunzo haya  wakatumie wakatumie elimu hiyo  kuleta matokeo bora katika maeneo yao ya kazi ikiwemo kukuza uchumi na kupunguza umasikini katika mikoa na halmashauri zao.

Akihitimisha kwa neno la shukurani kwa niaba ya washiriki wenzake Katibu Tawala Msaidizi Mipango na Uratibu kutoka Mkoa wa Ruvuma Bw. Edmundi Godwell Siame amesema yote yaliyoelekezwa na viongozi kupitia ufunguzi wa mafunzo hayo sambamba na elimu watakayoipata katika mafunzo hayo watayazingatia na  kufanyia kazi ili kuhakikisha taaluma yao inakuwa nyenzo muhimu katika kukuza uchumi wa Nchi.


Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Waziri Jafo ataka Zimamoto, Skauti wakomeshe majanga ya moto shuleni

    February 26, 2021
  • Vikundi 13 Wilayani Kibaha vyanufaika na mikopo ya sh milioni 46

    February 25, 2021
  • Magufuli: Viongozi tatueni kero za wananchi kwa wakati

    February 25, 2021
  • Shilingi Bilioni 3 zakwamua Wanawake, Vijana na Walemavu Geita

    February 25, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.