• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu

Wakurugenzi simamieni ukusanyaji wa Mapato

Imewekwa tar.: March 15th, 2020

Wakurugenzi wa Halmashauri zote nchini wameagizwa kuhakikisha wanasimamia ukusanyaji wa Mapato ya ndani ili kutimiza malengo yaliyopangwa na Serikali katika mwaka wa fedha wa 2019/2020

Agizo hilo limetolewa leo na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga alipokuwa akikagua  miradi ya maendeleo inayotekelezwa katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero Mkoani Morogoro.

Ameseama kuwa Mamlaka za Serikali za Mitaa zimepangiwa kukusanya  zaidi ya shilingi bilioni 765 kwa mwaka wa fedha 2019/2020 lakini hadi kufikia Februari, 2020 Mamlaka hizo zimeweza kukusanya mapato kwa asilimi 61 ya malengo ya mwaka.

“Inasikitisha kuona baadhi ya maeneo fedha za makusanyo ya mapato zinaingia mifukoni mwa watu, unakuta wanakusanya fedha lakini haziingii kwenye akaunti za Halmashauri, jambo hili linaisababishia Serikali kupoteza Mapato”Amesisitiza Mhandisi Nyamhanga.

Mhandisi Nyamhanga ameendelea kwa kusema kuwa ili Halmashauri ziweze kutekeleza mipango yake  na kufikia malengo waliojiwekea katika mwaka ni wajibu wa wakurugenzi wote kuweka nguvu katika kusimamia ukusanyaji wa mapato na kuzitumia fedha hizo  kwa kazi zilizopangwa.

 “Ongezeni kasi ya kukusanya mapato ya ndani, hakikisheni malengo mliyoweka ya ukusanyaji wa mapato yanatimizwa, zibeni mianya ya upotevu wa mapato hasa kwa watumishi wanaosimamia ukusanyaji huo, jambo hili linatia doa na kusababisha Halmashauri nyingi kutokamilisha  miradi ya maendeleo kwa wakati” Amesisitiza Mhandisi Nyamhanga.

Kuhusu matumizi ya fedha za ndani na ruzuku za Serikali Mhandisi Nyamhanga amesema Serikali inatoa fedha nyingi sana  katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa ajili ya utekelezaji wa miradi mbalimbali ya maendeleo ni wajibu wa Wakurugenzi wote nchini kuhakikisha wanasimamia matumizi ya fedha.

Amesema kuwa baadhi ya Halmashauri fedha hizo zinakusanywa lakini zinaanza kutumika kabla hazijaingizwa kwenye akaunti za Halmashauri, hii ni sawasawa na kutumia fedha mbichi hivyo naelekeza fedha hizo zikusanywe na kuingizwa kwenye akaunti ndipo zianze kutumika

Amefafanua kuwa Fedha nyingi zinakusanywa katika Halmashauri lakini haziingii kwenye Akaunti, Wakurugenzi hakikisheni  mnatumia mifumo ya kielektroniki kukusanya mapato na kuhakikisha fedha hizo zinaingia kwenye Halmashauri

Mhadisi nyamhanga amesema kuwa Halmashauri hazina budi  kuongeza kasi  ya ukusanyaji wa mapato ya ndani  lakini kupanga matumizi  mazuri ya fedha hizo  kama yalivyopangwa  kwenye bajeti zao .

Aidha amesisitiza kuwa Serikali imesambaza mashine  7227  kwenye Halmashauri mbalimbali nchini  kwa ajili ya kuboresha  ukusanyaji wa mapato ambapo ugawaji umeenda sambamba  na  uwezo wa Halmashauri katika kukusanya mapato.

Naye Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro Mhandisi Emmanuel Kalobelo amesema kuwa wameweza kudhibiti wizi wa mapato ya ndani kwa kuhakikisha matapeli wote wa Mapato wanatafutwa na kuzirudisha fedha hizo

Wakati huohuo Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga  amefanya ziara ya siku moja katika Halmashauri ya Wilaya ya Mvomero na kutembelea  mradi wa ujenzi wa Hospitali ya Wilaya Mvomero na mradi wa ujenzi wa Sekondari ya kumbukumbu ya Sokoine..

Na. Angela Msimbira MVOMERO



Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Waziri Jafo ataka Zimamoto, Skauti wakomeshe majanga ya moto shuleni

    February 26, 2021
  • Vikundi 13 Wilayani Kibaha vyanufaika na mikopo ya sh milioni 46

    February 25, 2021
  • Magufuli: Viongozi tatueni kero za wananchi kwa wakati

    February 25, 2021
  • Shilingi Bilioni 3 zakwamua Wanawake, Vijana na Walemavu Geita

    February 25, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.