• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Wadau PS3, GHSC TA – TZ, Waunga Mkono Juhudi za Serikali ya Awamu ya Tano

Imewekwa tar.: July 6th, 2019

Wadau wa Maendeleo nchini kupitia mradi wa Uimarishaji Mifumo katika Sekta za Umma (Public Sector Strengthening System-PS3) na (Global Supply Chain Technical Assistance Tanzania-GHSC TA – TZ), wameitikia wito wa serikali na kujitokeza katika kufanikisha zoezi la kuimarisha mfumo wa Uendeshaji wa Shughuli za Afya katika maeneo yote yakutolea huduma za Afya serikalini, ujulikanao (Government of Tanzania Health Operations Management Information System -GoTHOMIS). Wadau hao wameitika wito kufutia maelekezo ya Serikali kutaka mfumo huo uimarishwe kwa kuongezewa maeneo ya kiutendaji.

Akizungumza na Wadau wa Maendeleo mwanzoni mwa Mwezi Mei, 2019 Katibu Mkuu Wizara ya Afya Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt. Zainab Chaula, wakati wa kikao cha pamoja baina ya Wizara hiyo na ile ya Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) alisema, umefika muda kwa wadau kuungana na kujenga mfumo wa GoTHOMIS kwani mfumo huo umeonesha kuwa na tija na ufanisi kwenye nyanja ya Afya.

“Kwa Muda mrefu tumeshuhudia mifumo mbali mbali lakini yote hii ikiwa kwenye maeneo machache ya nchi ikifanywa kwa majaribio ambayo hata hivyo tija yake imekuwa sio yakuridhisha, alisema Chaula na kuongeza kuwa, suala lakutuambia unafanya shughuli ya Jamii halafu hatuoni tija ya unacho kifanya sio wakati wake kwa sasa, lazima wote tuungane na tukubali kutembea kwa pamoja na mfumo huu ambao umeonesha tija na ufanisi” alisema Dkt. Chaula.

Wito wa Katibu Mkuu huyo, ulikuja wakati ambapo tayari mfumo ulikuwa umesimikwa kwenye maeneo yakutolea huduma za afya yapatayo 383 ikiwepo Zahanati 91, Vituo vya Afya 180, Hospitali Teule za Wilaya 12, Hospitali za Wilaya 77 na Hospitali za Rufaa za Mikoa 23 na kufanya   asilimia 6 ya maeneo yote yakutolea huduma za afya nchini.

Akiwasilisha mada katika kikao hicho juu ya uboreshaji wa mfumo wa GoTHOMIS, Mkurugenzi wa TEHAMA Ofisi ya Rais TAMISEMI, Erick Kitali, alisema shabaha iliyo mbele yao nikuimarisha mfumo kwa kutumia wataalam wazawa na wanaamini katika nguvu ya pamoja ikiwepo kushirikiana na wadau wa maendeleo wote.

Akizungumza kando ya wataalam wanao endelea na kazi ya uimarishaji wa mfumo huo mkoani Morogoro, Mtaalam kutoka Global Supply Chain Tanzania, Alfredy Mchau, alisema wamewiwa kuunga mkono juhudi za serikali katika kuimarisha mfumo huo wa GoTHOMIS kwani ni moja ya vipaumbele vyao katika kushirikiana na serikali kuboresha huduma za Afya kwaajili ya upatikanaji wa taarifa sahihi na kwa wakati.

“Alipotoa wito Katibu Mkuu, kwa wadau juu ya kuunga mkono suala hili, sisi kama Global Supply Chain Technical Assistance Tanzania (GHSC TA – TZ), tulielewa nini dhamira ya Serikali hii ya awamu ya tano inayo ongozwa na Mhe. Dkt. John Pombe Magufuli, katika sekta   ya Afya, ambayo kimsingi ndio msingi wa maendeleo ya nchi yoyote.

Mchau aliongeza kuwa, GHSC TA – TZ ilikwisha anza harakati za uboreshai wa mfumo wa GoTHOMIS ili uweze kubadilishana taarifa na mfumo wa eLMIS ili kuboresha upatikanaji wa taarifa za dawa, vifaa tiba na vitendanishi nchi nzima hivyo tunaamini kwa nguvu hii ya pamoja tutapiga hatua kubwa katika kuihudumia jamii, kwani Umoja ni Nguvu na Utengano ni Udhaifu” alisisitiza Mchau.

Kwa upande wake mmoja wa wafanyakazi kutoka mradi wa kuimarisha Mifumo ya Sekta za Umma nchini PS3 Mhandisi, Revocutus Mtesigwa, alisema huo ni muendelezo wa juhudi ambazo wamekuwa nazo hususan katika uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma nchini.

“PS.3 Hii kwetu ni muendelezo wa shughuli ambayo tayari tulisha anza hapo awali, kwani tayari kuna maeneo yakutolea huduma za Afya yasiyo pungua 400 ikiwepo Hospitali, Vituo vya Afya na Zahanati  tumewezesha kufungwa kwa mfumo na unafanyakazi, maeneo ambayo kama mradi tuliokwisha fanyia kazi ni eneo la Mafunzo kwa watumiaji, ufungaji Miundombinu ya Mtandao Kiambo (Local Area Network-LAN), hivyo Kauli ya Katibu Mkuu kwetu ilituongezea chachu na ari yakuendelea kushirikiana zaidi na Serikali lakini pia Wadau wengine wa Maendeleo katika kujenga nchi.  

Serikali bado inaendelea kuwakaribisha wadau wa maendeleo kujitokeza kwaajili yakufanikisha uboreshaji wa Mfumo wa GoTHOMIS, ambao utakuwa Madhubuti na wenye tija katika ngazi zote za kutolea huduma za Afya nchini.

Anaandika Atley Kuni- TAMISEMI


Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Vikundi 47 Kondoa vyapewa mikopo ya shilingi milioni 147

    February 24, 2021
  • Mikopo ya Shilingi Milioni 85 yatolewa kwa Vikundi wilayani Bunda

    February 24, 2021
  • Mradi wa Fursa na Vikwazo Iliyoboreshwa Kuingizwa kwenye Majukumu ya OR - TAMISEMI

    February 23, 2021
  • Mikopo ya Sh. Milioni 850 yatolewa kwa Vikundi 104 jijini Tanga

    February 15, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.