• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Ushirikiano wa Viongozi na Watumishi Utaboresha Huduma kwa Wananchi

Imewekwa tar.: January 17th, 2019

Watumishi wa Umma wametakiwa kutumia sheria, taratibu, kanuni na busara katika kutekeleza majukumu ili kuleta ubora katika huduma wanazo zitoa kwa watanzania.

Hayo yamebainishwa leo na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI) Selemani Jafo katika hafla fupi ya kuwakaribisha Viongozi wapya na kuwaaga Viongozi waliokuwa katika ofisi hii.

Mhe. Jafo amesema ili kupata matokeo bora katika utendaji kazi wa mtumishi yeyeto lazima kujenga daraja la mahusiano mazuri na upendo baina yetu ili kuweza kutoa huduma stahiki kwa watanzania tunao wahudumia.

“Sisi Viongozi jukumu letu ni kuwahudumia watanzania na kuhakikisha wanapata huduma bora kutoka kwetu kwani wao ndio walio tupa dhamana hii ya kuwatumikia, bila wao sisi tusingekuwa na watu wa kuwahudumia” Amesema Jafo.

Jafo amesema kuwa yeye na timu nzima ya Ofisi ya Rais -TAMISEMI wanawakaribisha Katibu Mkuu OR - TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga na Naibu Katibu Mkuu (Afya) OR-TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima na kuwaahidi kutoa ushirikiano wa hali ya juu ili kuhakikisha wanapata matokeo zaidi katika utendaji kazi wa kuwahudumia wananchi.

Jafo ameongeza kuwa kuna haja ya Katibu Mkuu OR-TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga kukaa na wataalamu wake kuona ni namna gani wataboresha miundo mbinu ya barabara katika Halmashauri na Wilaya za nchi hii.

Kwa upande mwingine Jafo amesema kuwa anawapongeza sana Mhandisi Mussa Iyombe na Katibu Mkuu Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto Dkt.Zainabu Chaula kwa ushirikiano mzuri na utendaji bora waliyouonyesha kipindi walichohudumu katika Ofisi ya Rais - TAMISEMI na kuwatakia kila la kheri huko waendako.

Naibu Waziri anayeshughulikia Elimu OR - TAMISEMI Mwita Waitara amewataka watumishi kuwa mabalozi wazuri wa Serikali katika kutekeleza miradi mbali mbali inayotekelezwa na serikali hii.

“Kila mtumishi ni wajibu wake kuwa muadilifu katika kutekeleza miradi ya Umma na kila mtu atambue wajibu wake katika nafasi yake ili kuleta mapinduzi katika kukuza maendeleo ya nchi yetu” Amesema Waitala.

Kwa upande wake Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Joseph Nyamhanga ametoa wito kwa watumishi wa OR-TAMISEMI kumpa ushirikiano wakutosha katika kuboresha huduma za utekelezaji wa miradi ya Umma, kusimamia ukusanyaji wa mapato na kuhakikisha yanatumika vizuri katika kuwanufahisha watanzania kwani ni kodi zao.

Akitoa neno la kuwaaga na kuwashukuru watumishi na Viongozi wa OR TAMISEMI, Mhandisi Mussa Iyombe ametoa nasaha kwa watumishi wa Umma kwa kuwataka kutenda haki na kuwa wawazi katika kutekeleza majukumu yao ya kila siku kwani ndio silaha bora ya mtumishi Umma.

Naye Dkt.Chaula ametoa wito kwa watumishi wote kuwa na utayari wa kufanya kazi na mtu yeyote na sehemu yoyote kwani watumishi jukumu kubwa kwao ni utendaji na katika swala la uongozi ni mchezo wa kupokezana vijiti.

Awali akiwasalimia watumishi wa OR TAMISEMI Dkt. Dorothy Gwajima amesisitiza kuimarisha uratibu mzuri, uwazi, utekelezaji wa majukumu ili kujenga Serikali ya watu na kwa ajili ya maendeleo ya watanzania kwa ujumla.

                                Wanaandika Majid Abdulkarim na Fred Kibano

Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Vikundi 13 Wilayani Kibaha vyanufaika na mikopo ya sh milioni 46

    February 25, 2021
  • Magufuli: Viongozi tatueni kero za wananchi kwa wakati

    February 25, 2021
  • Shilingi Bilioni 3 zakwamua Wanawake, Vijana na Walemavu Geita

    February 25, 2021
  • Vikundi 47 Kondoa vyapewa mikopo ya shilingi milioni 147

    February 24, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.