• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Uboreshaji wa huduma za afya ya msingi ni chachu ya kuimarisha uchumi wa kati

Imewekwa tar.: August 3rd, 2020


Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa uboreshaji wa Huduma ya Afya msingi ni nguzo muhimu katika kuimarisha uchumi wa kati kwa kuwa  afya za watanzania ndio chachu ya kuongeza juhudi katika kufanya kazi ili kuinua uchumi wa Taifa.

Ameyasema hayo leo wakati akiwasilisha mrejesho kwa watanzania mafanikio ya miaka mitano ya maboresho ya huduma za afya Msingi katika Mamlaka za Serikali za Mitaa iliyofanyika katika ukumbi wa LAPF Jijini Dodoma.

Mhe. Jafo amejikuta akibubujikwa na machozi namna wananchi walivyo kuwa wakipata adha na kupoteza maisha kutoka na ukosefu wa huduma za afya kwenye baadhi ya maeneo nchini jambo lililokuwa linadhohofisha afya za wananchi katika utafutaji wao kutokana na kutokuwa na afya imara.

Amesema kuwa wananchi wengi wamekuwa  wakipoteza maisha kutokana na kukosa huduma bora za afya, lakini kwa kipindi cha miaka mitano ya Serikali chini ya Rais John Pombe  Magufuli imetoa kipaumbele kwa sekta hiyo na kuondoa adha kwa wananchi  hivyo kuchagiza katika utafutaji wa kipato .

“Watu wenye uwezo hawafahamu  kuwa kuna baadhi ya wananchi  walikuwa wakiteseka  kupata huduma za afya,  na walikuwa  wanasafiri zaidi ya kilometa  140  kutafuta huduma, wamama wajawazito walikuwa wakipata matatizo  ya fistula, baada ya kupata uchungu kwa muda mrefu hali hii ilisababisha vifo vingi katika jamii” ameeleza Mhe. Jafo.

Akiongelea kuhusu mafanikio yalipyopatikana katika utoaji wa huduma za afya ya msingi hasa katika ngazi za Mamlaka za Serikali za Mitaa Mhe. Jafo amesema  tangu uhuru  kulikuwa na hospitali 77 katika Halmashauri 185 jambo ambalo lilikuwa likilalamikiwa na wananchi kwa muda mrefu kuhusu  miundombinu ya Afya nchini.

Amewashukuru wataalam wa afya nchini  kwa kuhakikisha wanafanyakazi kwa weledi  na  “kuwa  injini ya kuhakikisha  wanatoa huduma bora kwa jamii na kupunguza changamoto zilizokuwepo awali na kupunguza malalamiko kwa wananchi.

Mhe. Jafo amefafanua kuwa baada ya kukarabati na kujenga vituo vya afya nchini  wakinamama wajawazito waliojifungua katika vituo hivyo vipya ni  219,764  na waliopata huduma ya upasuaji ni 18,826.na wagonjwa wengine zaidi ya 6000 walifanyiwa  upasuaji wa kawaida.

Aidha, katika siku ya afya ya TAMISEMI  Mhe Jafo aliweza kutembelea kituo cha afya  cha Makole, Jijini Dodoma  na kutoa zawadi  kwa wajawazito waliojifungua  katika kituo hicho kama ishara ya kuwapongeza kwa kuweza kupata huduma kwenye vituo vilivyokarabatiwa na kujengwa na Serikali.

Awali, Mwakilishiwa Katibu Mkuu Wizara  ya Afya,  Maendelo  ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Dk.Grace Maghembe, amesema kuwa kuna mikoa mitano ambayo haikuwa na  hospitali  za rufaa za Mikoa, lakini kwa sasa zimejengwa na zinatoa huduma katika ubora wa hali ya juu.

“Uboreshaji wa huduma za afya ikiwemo za kibingwa nchini umechangia kupunguza idadi ya wagonjwa wa kupelekwa nje ya nchi”, amesisitiza Maghembe.

Kwa upande wake  Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Afya katika Ofisi ya Rais TAMISEMI, Dk.Dorothy Gwajima amesema kuwa uwepo wa miundombinu hiyo inatakiwa kwenda  sambamba   na utoaji wa huduma bora kwa wananchi ili kuwa vutia watanzania wengi zaidi kujiunga na Mfuko wa Afya ya Jamii iliyoboreshwa(CHF).

Na Angela Msimbira OR-TAMISEMI

Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Bil 16.4/- zarejesha hadhi ya Shule za Sekondari za Ufundi nchini

    January 22, 2021
  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.