• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App

“Tuendelee kuliombea Taifa, Ndege yetu imeachiwa “Waziri Jafo.

Imewekwa tar.: September 4th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amewataka viongozi wa dini Nchini kote kuendelea kuliombea Taifa hasa wakati huu ambao miradi mikubwa ya maendeleo inatekelezwa.

Waziri Jafo ameyasema hayo wakati akifunga Mkutano wa 82 wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania unaofanyika chini ya Taasisi ya Huduma ya Kijamii za Kikristo(CSSC) katika ukumbi wa St. Gasper Jijini Dodoma.

Waziri Jafo amesema “Serikali ya Awamu ya Tano inatekeleza miradi mikubwa ambayo haijawahi kutokea tangu Uhuru, kila unapopita unaona ujenzi wa miundombinu ya barabara inaendelea, halkadhalika ujenzi wa reli ya kisasa (SGR), huku mradi wa ufuaji umeme wa mto Rufiji unatekelezwa hatuna budi kuendelea kumuombea Rais wetu Dkt. John Joseph Pombe Magufuli azidi kuwa na afya njema na aweze kusimamia miradi hii hadi ukamilifu wake”

Tunashukuru Mungu leo hii Mahakamu Kuu ya Gauteng, Africa Kusini imetoa hukumu na kuamuru ndege yetu ya Air Tanzania iliyokuwa inashikiliwa nchini humo iachiwe na mlalamikaji alipe gharama za kesi hizi ni habari njema sana kwetu na haya ni matunda ya kufanya vitu kwa nia njema na dhamira ya dhati ya kuwainua watanzania tusiache kuomba kwa ajili ya Taifa hili aliongeza Jafo.

Wakati huo huo Waziri Jafo aliziagiza Halmashauri zenye Hospitali  Teule (DDH) kuhakikisha wanafanya vikao na Taasisi za kidini zenye makubaliano ya uendeshaji wa Hospital hizo.  

“Hizi tabia za Halmashauri kusema hawana hela za vikao sjui viburudisho zisikwamishe ufanyikaji wa vikao, kutaneni hata saa nane mchana mpaka kumi jioni cha msingi mjadiliane changamoto zinazokabili hospitali hizo na kuzitaftia njia ya kuzitatua kwa pamoja” alisema Jafo.

Kuna changamoto ndogondogo ambazo zinaweza kutatuliwa kwa mashauriano tu lakini unapoziacha kwa muda mrefu zinakuwa tatizo kubwa, mkiwa mnakutana ni vizuri katika uboreshaji wa huduma za Afya kwenye  Halmashauri husika aliongeza Jafo.

“Taasisi za Dini mnafanya kazi kubwa sana katika Sekta ya Afya na kwa muda mrefu mmekuwa mkimiliki Hospital takribani 105 na Serikali tulikuwa na Hospital 77 tu kabla hatujaanza ujenzi wa Hospital za Wilaya 67.

Mmekuwa msaada katika kuwafikia wananchi ambao Serikali ilikua bado haijajenga Hospital niwapongeze kwa  kuhakikisha huduma za Afya zinapatikana karibu na wananchi na kwa haraka hakika mmewasaidia watanzania wetu kupata huduma bora za Afya  na mmeboresha afya zao Alisema Jafo.

Halkadhalika Waziri Jafo aliweka wazi mpango wa Serikali kukamilisha mchakato wa  kuajiri Watumishi wa Afya takribani 400 ambao kwa kiasi flani wataenda kupunguza uhaba wa watumishi wa Afya katika Vituo vya kiutolea huduma za Afya.

“Ninafahamu fika tatizo la uhaba wa watumishi katika hospital nyingi Serikali tunalifahamu hilo na tumechukua hatua za makusudi za kutangaza ajira za Afya na sasa tunakamilisha mchakato wa ajira hizo na muda si mrefu mtaanza kuwapokea kwenye baadhi ya Hospital ambao wataongeza nguvu katika utoaji wa huduma za Afya Nchini” Alisema Jafo.

Akizungumza katika Kikao hicho Rais wa Chama cha Madaktari wa Kikristo Tanzania Dr. Bwire Chirangi alitaja changamoto zinazowakabili ni pamoja na kukosa vikao vya mashauriano, uhaba wa watumishi wa Afya pamoja na miundombinu duni ya kuzifikia huduma za Afya.

Aidha Dr. Chirangi alieleza kuwa Chama hiki kimeanza mwaka 1937 na kinawakutanisha pamoja wataalamu wote wa Afya wanaohudumu katika Hospital za Dini na wamekuwa wakikutana kila mwaka kujadili changamoto na mafanikio mbalimbali ya huduma za Afya zinazotolewa na Taasisi za Dini ya Kikristo.



Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Natoa siku siku 12 mtatue kero za soko la Ndugai na Stendi kuu ya Mabasi- Waziri Jafo

    March 03, 2021
  • Agizo la ujenzi wa vyumba vya madarasa 2257 latekelezwa

    March 02, 2021
  • Waziri Jafo ataka Shilingi Bilioni 245 za Miradi ya Maendeleo zitumike kwa wakati

    March 01, 2021
  • Serikali yalegeza masharti mikopo ya asilimia 10

    February 27, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.