• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App

Tsh. Bil 77 za Mradi wa Tscp zatekeleza Agizo Rais JPM Jijini Dodoma

Imewekwa tar.: June 26th, 2018


Mradi wa Mpango Miji Mkakati ‘Tanzania Strategic Cities Project’ maarufu kama Tscp unaosimamiwa na Ofisi ya Rais TAMISEMI umetekeleza Agizo la Rais Dkt. John Pombe Magufuli kwa kutoa Fedha zaidi ya Tsh. Bil 77 kwa ajili ya kujenga miundombinu katika Jiji la Dodoma.

Akizungumza katika hafla ya utiaji  saini  miradi hiyo itakayotekelezwa kupitia mradi wa Tscp  Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais  Tamisemi Mhe. Selemani Jafo amesema mradi huu wa kimkakati umelenga kubadilisha kabisa muonekano wa Jiji la Dodoma kwa kutekeleza yale aliyoagiza Mhe.Rais alipotangaza kuipandisha  hadhi iliyokuwa Manispaa ya Dodoma kuwa Jiji.

“Jiji hili lazima liwe la tofauti, lenye hadhi ya Makao Makuuu ya Nchi na livutie kuliko majiji yote Tanzania, tutaweka miundombinu ambayo itabadilisha kabisa muonekano wa Jiji, itaongeza  fursa za biashara na kuwapunguzia kabisa adha wananchi wetu katika maeneo ambayo wamekuwa wakiyalalamikia.

Tunaimani  kupitia kazi itakayofanyika hapa  mtu aliyeondoka Dodoma mwaka huu akirudi baada ya miaka miwili tutamshika  mkono kumuelekeza mitaa ya Jiji la Dodoma, hapatakuwa kama palivyo sasa na mabadiliko yatayofanyika ni ya kimataifa” Alisema Jafo.

Kupitia hafla hiyo Mhe. Jafo aliwatahadharisha  wakandarasi washauri wa mradi  kusimamia mradi huo kwa mujibu wa taratibu na sheria na kuhahakisha thamani ya fedha inaonekana kwa kila kipengele kitakachotekelezwa.

“Mkandarasi mshauri  wajibu wenu  ni kuhakikisha kila kilichoainishwa kiinafanyika kwa wakati na kwa usahihi wakati huo huo kumshauri mteja wao ambaye ni Halmashuri kufanya yale yote yanayotakiwa ili kazi iende sawa na kumsimamia mkandarasi kufanya kazi hiyo kwa ubora wa hali ya juu na endapo utaenda kinyume na haya Wizara yangu haitasita kukuchukulia hatua kwa mujibu wa sharia” alisema Jafo.

Alimazia kuwa Ofisi ya Rais TAMISEMI inatekeleza miradi mikubwa mitatu kwa fedha za mkopo toka Benki ya Dunia yenye lengo la kuimarisha na kuboresha Halmashauri za Majiji, Manispaa, Miji pamoja na Mkoa mzima wa Dar es Salamm ili mamlaka hizo ziweze kukua kulingana mabadiliko tunayokwenda nayo kuelekea uchumi wa kati na  ziweze kutoa huduma bora kwa wananchi wake.

Jafo alitaja miradi mikubwa ya miundombinu inayosimamiwa na Ofisi yake kuwa ni Mradi wa Mpango Miji Mkakati (Tscp) unatekelezwa kwenye Majiji na Manispaa 8 na Dodoma ikiwa ndani ya mradi huu ambao  utagharimu jumla ya fedha za kitanzania sh Bil 840, Mradi wa Uendelezaji wa Jiji la Dar es Salaam(Dmdp) ambao ni maalumu kwa kushughulikia changamoto za Jiji la Dar es salaam  nao utagharimu Tsh. Bil 660 pamoja na Mradi wa Uendelezaji na Uboreshaji wa Halmashauri za Miji(Ulgsp) unatekelezwa katika Miji 18 na unagharimu Tsh. Bil. 650.  

Naye Naibu Waziri Ofisi ya Waziri Mkuu Sera,Bunge,Kazi,Vijana, Ajira na Watu wenye Ulemavu ambaye pia ni Mbunge wa Dodoma Mhe. Antony Mavunde akizungumza katika hafla ya utiaji saini wa miradi ya miundombinu katika Jiji la Dodoma ameishukuru Serikali kwa kuleta Fedha kwa ajili ya ujenzi wa miradi itakayofungua  milango ya maendeleo katika Jiji la Dodoma.

Pia aliwakumbusha wananchi wa Dodoma kuitumia fursa hii ya upatikanaji wa miradi mikubwa kama chachu ya maendeleo ambayo itakuza uchumi wa mtu mmoja mmoja na Taifa kwa ujumla na kubadilisha maisha kutoka yalivyo sasa na kuwa bora zaidi.

Nanye Mkuu wa Mkoa wa Dodoma Mhe. Bilinith Mahenge amesema miradi hii ni fedha nyingi sana na Serikali imeamua kuwekeza katika Jiji hili hivyo yeye kama msimamizi Mkuu wa shughuli za Mkoa huu atahakikisha atasimamia kwa karibu miradi hii ili  ikamilike kwa wakati na kwa ubora wa hali ya juu.

Akiwasilisha taarifa mradi Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi ametaja kazi zitakazofanyika kupitia mradi wa TSCP kuwa ni Ujenzi wa barabara za Lami Km 26.6, Taa za barabrani  913, mfereji mkubwa wa kusafirishia maji ya mvua Km 6.5, Ujenzi wa Stendi ya Kisasa, Soko kuu la Kisasa, vizimba 7 vya kukusanyia taka, kituo kikuu cha kuegeshea malori pamoja na bustani ya kupumzikia yenye viwanja mbalimbali vya michezo.

Aliongeza kuwa barabara za lami zitajengwa maeneo ya katikati ya mji, pembezoni pamoja na barabara moja kubwa ya mchepuko zitajengwa kwa kiwango cha Lami Ngumu (Concret Asphat) na zitakuwa na  eneo la waenda kwa miguu, mifereji ya maji ya mvua pamoja na Taa za barabara zinazotumia nguvu ya jua.

Akizungumzia ujenzi wa stendi ya kisasa itakayojengwa eneo la Nzuguni Kunambi amesema itajengwa kwenye eneo lenye ukubwa wa Ekari 87 itakua na uwezo wa kuegesha  Mabasi Makubwa 250, Mabasi madogo na magari ndogo 600, Bajaji 300 na pia itakua na maeneo makubwa ya biashara pamoja na eneo maalumu kwa ajili ya wafanyabiashara ndogondogo (Machinga) pamoja na mama lishe.

Kazi hii inaanza rasmi Julai Mosi,2018 na itachukua muda wa miezi 15 hadi kukamilika kwake.

Anaandika Nteghenjwa Hosseah, OR-TAMISEMI.

Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Uhaba wa Saruji wachelewesha ujenzi wa barabara za Mji wa Serikali

    March 03, 2021
  • Natoa siku siku 12 mtatue kero za soko la Ndugai na Stendi kuu ya Mabasi- Waziri Jafo

    March 03, 2021
  • Agizo la ujenzi wa vyumba vya madarasa 2257 latekelezwa

    March 02, 2021
  • Waziri Jafo ataka Shilingi Bilioni 245 za Miradi ya Maendeleo zitumike kwa wakati

    March 01, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.