• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Serikali yatoa ufafanuzi wa hoja, ajira mpya za waalimu.

Imewekwa tar.: November 30th, 2020

Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhandisi Joseph Nyamhanga, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimeti ya utumishi wa umma na utawala bora Dkt. Laurean Ndumbaro na Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo wametoa ufafanuzi juu ya hoja mbalimbali zilizojitokeza kwenye ajira mpya za waalimu.

Ufafanuzi huo umetolewa leo katika Ofisi ya Rais – TAMISEMI Jijini Dodoma  mara baada  kutokea hoja mbalimbali katika mitandao ya kijamii na vyombo vya habari  kuhusu ajira  mpya za walimu zilizotangazwa hivi karibuni.

Amesema ajira  hizo zilitangazwa  baada ya kukamilika kwa mchakato  wa uchambuzi  wa maombi  ya ajira  uliofanywa  na Ofisi ya Rais  TAMISEMI  kwa kushirikiana  na Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Ofisi ya Rais Menejimenti ya Utumishi  wa umma  na utawala bora na  tume  ya utumishi wa walimu.

Mhandisi Nyamhanga  amesema hoja kubwa ilyojitokeza ni kwa jina la  Mwalimu mmoja kujitokeza katika kila ukurasa na kuonekana mara 196, badala ya mstari wa  maelezo ya Jedwali (Sub- titles) lakini shule aliyopangiwa ni moja, pamoja na jina hilo kujirudia  halikuchukua nafasi   ya mwombaji  yoyote  ya walimu waliotakiwa kuajiriwa au kuathiri  idadi ya waalimu  waliotakiwa kuajiriwa na  tayari marekebisho yamefanyika.

Mhandisi Nyamhanga amefafanua kuwa Shule binafsi kupangiwa mwalimu, Serikali imekuwa ikiingia ubia na baadhi ya Shule binafsi ambazo hupokea  wanafunzi wenye uhitaji maalum, shule hizo hupamgiwa  walimu na  kupewa ruzuku ya uendeshaji hivyo Shule ya Mwalimu Tutuba ilikuwa katika mchakato wa kuingia  ubia na serikali lakini haukukamilika, hivyo Serikali baada ya  kujiridhisha mwalimu aliyepangiwa katika shule hiyo amepangiwa  katika shule ya sekondari Malagarasi.

Kwa upande wa  wahitimu waliomaliza kidato cha nne mwaka 2017, 2018 na 2019 kupangiwa vituo vya kazi Mhandisi Nyamhanga ameeleza  waombaji wa ajira walitumia  mwaka wa kuhitimu chuo badala  ya mwaka wa kuhitimu  kidato cha nne ambapo waombaji 27 waliandika mwaka 2019, waombaji 27 waliandika mwaka 2019 na waombaji 13 waliandika mwaka 2017, Serikali ilihakiki vyeti vyao  na kubaini  kuwa waombaji hao walihitimu  kidato cha nne kati ya mwaka 2010 hadi 2014.

Kwa kuongezea amesema kuwa Serikali imefuata  utaratibu wa kuhakikisha Waombaji wote waliopata nafasi ya ajira wanazingatia  vigezo vilivyotolewa  katika tangazo la ajira ambapo lilifafanua kuwa mwombaji asizidi umri wa miaka 45.

Aidha Mhandisi Nyamhanga amewalekeza  Wakurugenzi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakiki vyeti halisi  vya waliopata ajira na kujiridhisha  kabla ya kutoa barua  za ajira, na kusisitiza kuwa endapo  itabainika  udanganyifu au kasoro za vyeti vya kitaaluma  wahusika watachukuliwa hatua za kisheria.

Kwa upande wake, Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Menejimeti ya utumishi wa umma na utawala bora Dkt. Laurean Ndumbaro amesema  Serikali imetoa ajira za waalimu kwa awamu mbili ambapo awamu ya kwanza  wametoa ajira 8000 na awamu ya pili watatoa kwa waalimu  5000  ili kupunguza malimbikizo ya mshahara kwa waalimu wapya.

Naye Katibu Mkuu Wizara ya Elimu, Sayansi na Teknolojia, Dkt. Leonard Akwilapo ameweka wazi kuwa Serikali itahakikisha waalimu wote waliomba ajira kwa masomo waliyoomba yanaendana na masomo wanayoyafundisha.






Matangazo

  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Tangazo la kazi kada ya Afya January 20, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

    January 11, 2021
  • Mweli awatega Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu kwenye Mfumo wa PREM/PREMS.

    January 10, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.