• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Serikali yataka uwazi kwenye matumizi ya Tsh. 12 bilioni za Mradi wa USAID Boresha Afya

Imewekwa tar.: October 18th, 2018

Na Mathew Kwembe, Dodoma

Naibu katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt Zainab Chaula amewataka Wakurugenzi kutoka Halmashauri 44 zilizo kwenye mradi wa USAID Boresha Afya kanda ya Kaskazini na kati kuhakikisha kuwa fedha zote zinazosaidia jitihada za serikali katika kuboresha sekta ya afya zinaonekana katika mipango kazi ya halmashauri zao.

 Akizungumza kwenye hafla fupi ya kutiliana saini mikataba na matumizi ya fedha za mradi kwa mwaka wa fedha 2018/2019 kwa viongozi wa wilaya nane za mkoa wa Dodoma ambao walitia saini mikataba ya halmashauri zao, na kuwawakilisha wenzao kutoka wilaya nyingine 37, Dkt Chaula alisema kuwa kwa kufanya hivyo kutaondoa changamoto za kiutendaji na kuongeza uwazi na uwajibikaji katika usimamiaji wa fedha zinazotolewa na wadau wa maendeleo katika miradi ya afya kwenye wilaya hizo.

Aliongeza kuwa wadau wengi wa maendeleo wanapobuni miradi ya afya hawashirikishi ngazi mbalimbali za serikali na hivyo wadau hawa kushindwa kuvielewa na kutekeleza vipaumbele vya serikali.

Hata hivyo Dkt Chaula aliusifu mradi wa USAID Boresha Afya kanda ya kati na Kaskazini kwa kuwa wazi na kuweka fedha za mradi katika halmashauri husika.

Mapema Mkurugenzi Mkazi wa Shirika lisilo la Kiserikali la Elizabeth Glaser linalopambana na na VVU/UKIMWI kwa watoto bwana Nelson Ojanji amemweleza Naibu Katibu Mkuu kuwa katika kipindi cha mwaka 2018/19 zaidi ya shilingi bilioni 12 zitatolewa kwa halmashauri 44 zinazotekeleza afua za Kifua Kikuu na Uzazi wa mpango.

“Bajeti za halmashauri washirika wa USAID Boresha Afya zote ziko tayari na viongozi wake watatia saini wakiwa katika halmashauri zao,” alisema Bwana Ojanji

Aidha katika kipindi cha mwaka 2017/2018, bwana Ojanji alisema kuwa zaidi ya shilingi bilioni 11 zilitolewa na Mradi huo kwa halmashauri 44 nchini ambako mradi huo unafanya kazi.

Alisema fedha hizo huwekwa kwenye mipango kazi ya idara za afya za halmashauri hivyo kuzipa halmashauri uwezo wa kupanga na kusimamia matumizi ya fedha na utekelezaji wa kazi za mradi.

Pamoja na kutoa fedhakwa halmashauri USAID Boresha Afya imetoa vifaa tiba mbalimbali vyenye thamani ya zaidi ya shilingi bilioni 3 katika halmashauri zote 44 zinazotekeleza mradi.

Halmashauri zinazotekeleza mradi wa USAID Boresha Afya kanda ya kati na kaskazini ni za kutoka mikoa ya Arusha, Dodoma, Kilimanjaro, Manyara, Singida na Tabora.

Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Asilimia 10 inavyoibua Wajasiriamali Arusha

    January 19, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.