• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App

Serikali yataka Shule za Sekondari zipewe kipaumbele ufadhili wa maabara za kompyuta

Imewekwa tar.: October 29th, 2018


Na Mathew Kwembe

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe.Selemani Jafo ameutaka Mfuko wa Mawasiliano kwa wote kuangalia uwezekano wa kuzisaidia shule za msingi na sekondari nchini kuwa na kompyuta ili kuwawezesha wanafunzi kutoachwa nyuma na maendeleo ya Teknolojia ya Habari na Mawasiliano

Akizungumza wakati wa ufunguzi wa mafunzo ya TEHAMA kwa walimu wa shule za msingi na sekondari kutoka mikoa 14 nchini yanayofanyika katika chuo cha Teknolojia ya Habari, Mawasiliano na Sayansi kilichopo ndani ya Chuo Kikuu cha Dodoma, Mhe.Jafo alisema kuwa ni muhimu kwa shule zote za sekondari nchini kuwa na maabara ya kompyuta ili kuwawezesha wanafunzi kujifunza kwa vitendo matumizi ya TEHAMA.

Alisema kwa kuanzia angependa kuona mfuko wa mawasiliano kwa wote unafadhili maabara za kompyuta kwa shule zote za sekondari nchini ili wanafunzi wapate elimu ya TEHAMA itakayowawezesha kupambana katika ulimwengu wa sayansi na Teknolojia ya Habari na Mawasiliano.

“Niombe mfuko mtafute namna ya kuzisaidia shule zetu za sekondari zipate kompyuta. Kila sekondari iwe na kompyuta lab, twende awamu kwa awamu,”alisema Mhe.Jafo na kuongeza kuwa  ifike muda kila shule ya sekondari nchini iwe na maabara ya kompyuta.

Alisema kuwa serikali kupitia Ofisi ya Rais TAMISEMI inalenga kuleta mapinduzi ya Elimu Tanzania kwa kuhakikisha kuwa inaboresha miundombinu ya shule na vifaa vya kufundishia na kujifunzia ili kuendana na matakwa ya sera ya elimu ya mwaka 2014

Kwa mujibu wa   sera hiyo,  Elimu ya Sayansi na Teknolojia ni muhimu katika kumuwezesha mwananchi kumudu mazingira yake na kumwezesha kuchangia maendeleo ya Taifa.

Aidha Waziri Jafo aliwataka Maafisa Elimu wa Mikoa na Wilaya kuhakikisha kuwa walimu wote 578 watakaopata mafunzo ya TEHAMA kutoka mikoa 26 ya Tanzania Bara na Mikoa 5 ya Zanzibar  wanayatumia mafunzo hayo kwa malengo yaliyokusudiwa.

Alisema kuwa hatarajii kuona maafisa elimu hao wanakuwa kikwazo kwa walimu waliopata mafunzo haya kitakachowafanya washindwe kwenda kutoa elimu kwa walengwa kama ilivyokusudiwa kwenye uandaaji wa mafunzo hayo.

Pia aliwaagiza wakurugenzi wa Halmashauri  kuhakikisha kuwa wanasimamia utekelezaji wa mpango huo kwa kuhakikisha kuwa hakuna kompyuta lab hata moja itafungwa kwa sababu mbalimbali.

“Sitaki kusikia shule ina kompyuta lab halafu  imefungwa,  nataka kuona shule zote zinatumia kompyuta lab kwa lengo la kuwawezesha wanafunzi waendane na kasi ya mabadiliko ya Sayansi na Teknolojia ya habari,” alisema.

Mapema mwakilishi wa Mtendaji Mkuu wa Mfuko wa Mawasiliano kwa wote Mhandisi Albert Richard alieleza lengo la mafunzo hayo ni kuwawezesha walimu wa shule za msingi na shule za sekondari wanaofundisha somo la TEHAMA waweze kutatua changamoto mbalimbali za mifumo ya habari na mawasiliano  zilizokuwa zikiwakabili wakati wa ufundishaji wa somo hilo.

Pia ni kuwajengea uwezo walimu ili waweze kutumia na kufanya marekebisho ya vifaa mbalimbali vya TEHAMA vilivyopo kwenye shule.

Jumla ya washiriki 289 kutoka mikoa 14 ya Tanzania Bara wanahudhuria mafunzo hayo yanayofanyika katika chuo kikuu cha Dodoma.

Mikoa inayoshiriki mafunzo hayo ni pamoja na Arusha, Dodoma, Geita, Iringa, Kagera, Kigoma, Kilimanjaro, Mara na Morogoro.

Mikoa mingine ni Mwanza, shinyanga, Simiyu, Singida na Tabora.

Mfuko wa Mawasiliano kwa wote ulianzishwa mwaka 2006 na kuanza rasmi mwaka 2009.

Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Kafanyeni Tohara kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi

    March 04, 2021
  • Uhaba wa Saruji wachelewesha ujenzi wa barabara za Mji wa Serikali

    March 03, 2021
  • Natoa siku siku 12 mtatue kero za soko la Ndugai na Stendi kuu ya Mabasi- Waziri Jafo

    March 03, 2021
  • Agizo la ujenzi wa vyumba vya madarasa 2257 latekelezwa

    March 02, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.