• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App

Serikali yataka Halmashauri ya Njombe kuongeza kasi ujenzi wa hospitali

Imewekwa tar.: May 3rd, 2019

Na Mathew Kwembe, Njombe

Serikali imeutaka uongozi wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe kuongeza kasi katika ujenzi wa majengo yake saba ya Hospitali mpya ya Halmashauri hiyo ambapo, majengo sita kati ya saba yapo katika hatua ya msingi.

Akizungumza na Uongozi wa Timu ya Uendeshaji Huduma za Afya ya Halmashauri ya Wilaya hiyo na Mkoa wa Njombe ambao, kwa pamoja walitembelea eneo la Matembwe lililopo umbali wa kilometa 65 kutoka Mji wa Njombe, Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Afya Dkt. Dorothy Gwajima amesema kuwa, ukiacha jengo la kutoa huduma za vipimo vya mionzi, majengo mengine yote sita bado yapo katika hatua ya msingi na ya umwagaji wa zege na hatua hii ni kinyume na kasi ya matarajio ya Serikali kuwa, majengo yote yawe yamekamilika ifikapo tarehe 30 Juni, 2019.

Kufuatia hali hiyo, Dkt Gwajima amemtaka Meneja wa TARURA anayesimamia ujenzi huo Mhandisi Samson Kalesi kuhakikisha kuwa anamsimamia mkandarasi anayejenga majengo hayo ili aongeze idadi ya mafundi ukilinganisha na waliopo sasa kwa ajili ya kuongeza kasi ya ujenzi wa majengo hayo na kuhakikisha yanakamilika mapema kama ilivyokusudiwa.

Dkt. Gwajima ameiagiza Halmashauri kuhakikisha kila wiki iwe inampatia taarifa za ujenzi wa hospitali hiyo ikiwemo picha zinazoonesha hatua iliyofikiwa kwa kila jengo. Aidha, ameagiza kuwe na daftari la taarifa fupi ya ujenzi uliofanyika kila jengo kila siku na taarifa hiyo itumwe pamoja na picha za majengo hayo. Aidha, ameagiza sambamba na kitabu cha Wageni na Viongozi wanaotembelea mradi huo pia, kuwe na daftari linalorekodi maelekezo na ushauri uliotolewa ili, kuweka kumbukumbu nzuri za ushiriki wao katika kufuatilia utekelezaji wa mradi huo.

Vilevile, Dkt Gwajima ameagiza Halmashauri kuhakikisha Kamati zote za Usimamizi wa Ujenzi huo zinafanya Vikao na kutunza muhtasari zote ili, kila inapohitajika kumbukumbu hizo zipatikane. Aidha, amesisitiza kuwa, katika Vikao hivyo uwakilishi wa wataalamu wa afya uzingatiwe ili, waweze kutoa ushauri wao kwa ajili ya kuwezesha kuepuka kasoro za kujenga bila kuzingatia ubora wa maeneo ya kitaalamu kwa kuwa katika huduma za hospitali kila eneo lina kanuni zake mahususi. Dkt. Gwajima amezitaja Kamati hizo kuwa ni Kamati ya Ujenzi, Manunuzi ya vifaa na Mapokezi ya Vifaa.

Pia, Naibu katibu Mkuu amesisitiza umuhimu wa majengo hayo kujengwa katika ubora unaotakiwa kwa kuzingatia ramani “DMO (Mganga wa Wilaya) hakikisha majengo yote saba yanajengwa katika ubora unaotakiwa, na kuepuka kuanza kufanya marekebisho kutokana na kukosekana kwa ufuatiliaji wa kitaalamu wakati wa ujenzi“ amesema Dkt Gwajima.

Kwa upande wake Mhandisi Kalesi amemhakikishia Naibu Katibu Mkuu kuwa, pamoja na uwepo wa changamoto kadhaa walizopitia wakati wa utekelezaji wa mradi huu, atahakikisha wanazingatia maelekezo yote aliyowapa na kuongeza kasi ya ujenzi. Aidha, Dkt. Gwajima ameupongeza Uongozi wa TARURA kwa kushirikiana katika utekelezaji wa mradi huu na kuziba pengo la upungufu wa Wahandisi licha ya majukumu makubwa waliyonayo. Aidha, Dkt. Gwajima ametambua ushirikiano huu na kusisitiza uendelee katika halmashauri zote wanazotekeleza miradi kama hii.

Mapema akisoma taarifa ya ujenzi wa Hospitali hiyo, Mganga Mkuu wa Halmashauri ya Wilaya ya Njombe Dkt Deusdedit Kalaso amemweleza Naibu Katibu Mkuu kuwa halmashauri hiyo imepokea fedha kiasi cha shilingi bilioni 1.5 kwa ajili ya ujenzi ambapo majengo yaliyopendekezwa kujengwa kwa fedha hizo ni pamoja na jengo la utawala, wagonjwa wa nje, stoo ya dawa, maabara, vipimo vya mionzi, jengo la kufulia nguo na jengo la huduma ya uzazi. Dkt Kalaso ameongeza kuwa, kufikia sasa halmashauri imetumia shilingi milioni 418.4 ambayo ni sawa na asilimia 28 ya matumizi ya fedha yote ya mradi na kwamba, hivi sasa taratibu za manunuzi ya vifaa vya ujenzi zinaendelea kwa kutumia fedha iliyobaki.

Wakati huo huo Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ys Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt Dorothy Gwajima jana alipata fursa ya kutembelea Kituo cha Afya Lupembe kilichopo katika Wilaya ya Njombe na kujionea hali ya utoaji huduma. Akiwa katika kituo hicho, Dkt. Gwajima amesikitishwa na hali isiyoridhisha ya mazingira ya kituo ikiwemo hali ya usafi na uwajibikaji kwa ujumla ambapo, amezitaka timu za usimamizi na uendeshaji wa huduma za afya mkoa na halmashauri (RHMT na CHMT) kutekeleza jukumu lao la kufuatilia na kusimamia mwenendo wa utoaji huduma huduma katika vituo vya afya na kuleta mabadiliko ya uwajibikaji vinginevyo, wazembe atawaondoa katika majukumu ya uongozi maana inaonekana hawatumii muda wao kufuatilia hali ya huduma katika vituo.

Kufuatia hali hiyo, Naibu Katibu Mkuu ameitaka RHMT na CHMT husika kujitathmini juu ya utendaji wao kwani kituo hicho kipo karibu zaidi na ofisi zao na kungekuwa na fursa kubwa zaidi ya kuwezesha ufuatiliaji lakini sivyo ambavyo imekuwa.

Aidha Dkt Gwajima alipata fursa ya kuongea na baadhi ya wateja waliokuwa kituoni ambao, nao walitoa maoni na kero zao ikiwemo hali duni ya usafi, majibu yasiyo rafiki ya watoa huduma na ukosefu wa baadhi ya dawa. Vilevile, Dkt. Gwajima alifanya mapitio ya takwimu mbalimbali za huduma ambapo baadhi ya aliyobaini kwa ufupi ni pamoja na uzembe katika ufuatiliaji wa wagonjwa hususan siku za mwisho wa wiki na mapumziko ya kazi, ukosefu wa baadhi ya vipimo na ukosefu wa kumbukumbu stahiki za dawa.

Dkt. Gwajima ameagiza maboresho katika kituo hicho yafanyike mara moja na kwamba, mapungufu anayokutana nayo katika vituo ni madogo na ambayo alishayatolea maelekezo na yalitakiwa kubainiwa na timu husika za usimamizi na uendeshaji huduma za afya katika mkoa na halmashauri husika.

Dkt. Gwajima amesema, kwa ujumla timu za usimamizi na uendeshaji huduma za afya mikoa na halmashauri (RHMT na CHMT) zikumbuke kuwa, ubora wa huduma za afya katika vituo ndiyo kioo pekee cha uwajibikaji wao hivyo, wajipange kuhakikisha wanatumia nguvu zaidi na muda zaidi kwa ajili ya ufuatiliaji wa huduma.

Aidha, Dkt. Gwajima amesema, timu itakayobainiwa kushindwa kufuatilia mwenendo wa utoaji huduma katika vituo na kuchukua hatua itambue kuwa, timu hiyo itakuwa imepoteza sifa za kuendelea na majukumu ya uongozi.

Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Uhaba wa Saruji wachelewesha ujenzi wa barabara za Mji wa Serikali

    March 03, 2021
  • Natoa siku siku 12 mtatue kero za soko la Ndugai na Stendi kuu ya Mabasi- Waziri Jafo

    March 03, 2021
  • Agizo la ujenzi wa vyumba vya madarasa 2257 latekelezwa

    March 02, 2021
  • Waziri Jafo ataka Shilingi Bilioni 245 za Miradi ya Maendeleo zitumike kwa wakati

    March 01, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.