• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App

Serikali yaagiza kufanyika kwa Sensa na Tathmini ya Utendaji wa wataalam wa afya.

Imewekwa tar.: November 23rd, 2020

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) anayeshughulikia Afya, Dkt. Dorothy Gwajima ameagiza Halmashauri zote nchini kufanya sensa  na tathmini ya wataalamu wa afya  waliopo katika vituo vya kutolea huduma za Afya ili kujua iwapo kila mtaalamu anafanya kazi zake kikamilifu bila vikwazo vyovyote.

Dkt. Gwajima ameagiza hayo hivi karibuni wakati alipokutana na watumishi wa kituo cha afya Town Clinic Mpanda mkoani Katavi ambapo amebaini kuwepo kwa mtaalamu wa afya ya kinywa na meno ambaye hatumiki kikamilifu kutokana na changamoto ndogo zilizo ndani ya uwezo wa Halmashauri.

Dkt. Gwajima ameeleza kuwa lengo la kufanya sensa hiyo ni kubaini mapungufu ambayo yamekuwa yakichelewa kujulikana na kuweza kufanya uwezeshaji kwa wataalamu ambao hawafanyi kazi zao kikamilifu kwa sababu mbalimbali ambazo nyingi ufumbuzi wake uko ndani ya uwezo wa Halmashauri.

Amefafanua kuwa  amekuwa akikutana na matukio kama haya kwenye maeneo kadhaa kitu kinachoashiria kuwa waajiri wanatakiwa kuimarisha ziadi ufuatiliaji wa wataalamu na kazi wanazotakiwa kufanyika kama zinafanyika kama ilivyokusudiwa na kama zipo changamoto ni zipi kwani nyingi wana uwezo wa kuzipatia majibu. .

Hata hivyo, amewapongeza Halmashauri ya Mji wa Mpanda kwa kuwa wabunifu katika kuhakikisha wanafanya uwekezaji wenye ubunifu kwa ajili ya kuhakikisha mtumishi huyo anatumika kutoa huduma kikamilifu.

“Wataalamu wetu wa afya wawezeshwe kwa wao kuwasilisha mipango yao hatua kwa hatua jinsi gani wataweza kupanuka kutoka hatua moja ya huduma kwenda ingine ukizingatia hizi ni nyakati za fursa ya uwepo wa Bima za Afya ikiwemo Mfuko wa Bima ya Afya ulioboreshwa (ICHF) hivyo, wananchi wanapochangia bima hizi wanachohitaji ni huduma”, amesema Dkt. Gwajima.

“Kwa hali hii lazima tubadilishe mitazamo yetu ya jinsi gani wananchi wananufaika na ajira tunazotoa siyo mtaalamu yupo huduma hakuna na anahitaji mahitaji machache tu tena yako ndani ya uwezo wa Halmashauri”, ameongeza Dkt. Gwajima.

Lakini pia Dkt. Gwajima ameelekeza timu za afya mikoa na halmashauri zote nchini kumiliki yaliyomo kwenye Ilani ya Uchaguzi Mkuu 2020 wa Chama kilichomo madarakani CCM ili ahadi zote zilizotolewa zitekelezwe kwa kasi na kwa wakati.

Dkt. Gwajima amesema kuwa maisha ya watanzania ya miaka mitano yako katika ilani hivyo ni wakati sahihi ya kila mtendaji kwa nafasi yake kutekeleza ilani hiyo kwa nguvu zake na akili zake zote maana yako mambo ambayo kila ngazi ya utekelezaji inaweza kuibuka na mpango wa utekelezaji wakati maelekezo ya mikakati mikubwa zaidi yakiendelea kutolewa.

“Ilani hii ndiyo mkataba na wananchi na sisi watendaji ndiyo tunaotekeleza hayo yatokee hivyo, mara baada ya Mhe. Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Dkt John Pombe Joseph Magufuli kuapishwa tayari hiyo ilikuwa ni ishara tosha ya kupulizwa kwa kipenga cha kuanza kutekeleza ilani kwa manufaa ya watanzania wote na taifa kwa ujumla”, amesisitiza Dkt. Gwajima.

Kwakuongezea Dkt. Gwajima amesema kuwa  kiongozi wa afya ngazi yoyote hadi kwenye vituo vya kutolea huduma za afya anapokuwa hajui kitu gani kimeandikwa kwenye Ilani hiyo kuhusu afya basi yeye atakuwa amegeuka kuwa tatizo katika kufikia malengo yaliyokusudiwa.

Dkt. Gwajima ameinisha moja ya majukumu yaliyopo katika Ilani hiyo ni kuhakikisha kila mwananchi anajiunga na bima ya afya ili kurahisisha upatikanaji wa huduma za afya hivyo, uhamasishaji wa wananchi kujiunga na bima hizo uende sambamba na wataalamu waliopo kuwezeshwa kutoa huduma.  


Matangazo

  • Badili Tahasusi kwa Wanafunzi Kidato cha Tano Tarajali na Vyuo vya Kati March 29, 2021
  • Kitabu cha Maombolezo ya Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Hayati Mhe. John Pombe Joseph Magufuli March 18, 2021
  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Watendaji Halmashauri watakiwa kujenga ushirikino na madiwani

    April 15, 2021
  • Tutayaendeleza yaliyoanzishwa na Hayati Dkt. John Pombe Magufuli – Waziri Ummy

    April 15, 2021
  • TARURA Iringa watumia shilingi milioni 153 kukarabati barabara za Kalenga

    April 12, 2021
  • Shilingi bilioni 1.5 zatumika kujenga vituo vinne vya afya Tunduru

    April 12, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.