• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Serikali yaagiza Halmashauri kutenga Maeneo kwa ajili ya Wamachinga

Imewekwa tar.: May 31st, 2018

Wakuu wa Wilaya nchini wameagizwa kuzisimamia halmashauri zilizo chini ya mamlaka zao za utawala kutenga maeneo maalum ya kufanyia biashara ndogondogo (machinga) ili wafanyabiashara hao waweze kuendesha shughuli zao bila kuvunja sheria, kanuni na taratibu zilizowekwa na serikali.

Agizo hilo limetolewa na Waziri wa nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo wakati akifungua Mkutano Mkuu wa Shirika la umoja wa wamachinga Tanzania – SHIUMA uliofanyika leo katika ukumbi wa shule ya Sekondari ya Dodoma, Jijini Dodoma.

Alisema Wakuu wa Wilaya wana wajibu wa kuratibu na kuhakikisha kuwa maeneo ya kufanyia bishara kwa wamachinga yanatengwa na Halmashauri ili kuwawezesha kufanya kazi zao kwa utaratibu bila kuvunja sheria za nchi.

Aliongeza kuwa wamachinga ni watu muhimu katika kukuza uchumi wa Tanzania kwa kuwa wafanyabiashara wadogo ndio wanaoleta muunganiko wa watu katika kada mbalimbali wakiwemo wasomi wenye shahada, astashaada, kidato cha sita, kidato cha nne, darasa la saba na wasiosoma kabisa wote huunganika na kufanyabiashara kama wamachinga.

Alisema kati ya watanzania milioni 50, walioajiriwa serikalini na sekta ya umma ni 520,000, hivyo kundi kubwa ni la watu ambao ama wamejiajiri au wameajiriwa katika sekta binafsi.

“Lakini kundi kubwa ni wale watu wanaojishughulisha kwa kutafuta riziki zao wenyewe ambao watu hao ndio unapata asilimia kubwa wako katika kundi la wamachinga,” alisema Mhe.Jafo na kuongeza:

“Utakuta mtu anafanyabishara katika mazingira magumu ambayo yanamfanya kila wakati kutokuwa na uhakika wa kupata kipato cha siku jambo ambalo linaathiri familia yake na kuongeza umaskini nchini, hivyo ifike mahali wakuu wa Wilaya waweke mikakati ya kuhakikisha wamachinga wote wanapatiwa maeneo bora ya kufanyia biashara ili wajikwamue kiuchumi, “alisisitiza Waziri

Aliongeza kuwa Serikali imejiwekea mkakati wa kutengeneza masoko mazuri na ya kisasa kwa kuweza kuweka mazingira bora kwa wamachinga kufanya biashara zao katika maeneo stahiki.

Aidha Waziri Jafo alisema kuwa Viongozi wanatakiwa kutafakari na kutatua kero ya maeneo kwa ajili ya kufanyia biashara wamachinga, hivyo serikali imeanza mpango mkakati wa ujenzi wa masoko mazuri ya kisasa ili wafanyabishara waweze kufanya kazi katika mazingira bora na tayari imetenga shilingi bilioni 149 kwa ajili ya ujenzi wa masoko, stendi za kisasa na viwanda vidogo.

“Nimetoa maagizo soko lolote litakalojengwa lazima mustakabali wa wafanyabiashara wadogo wadogo waliokuwepo awali umejulikana na kuwa kipaumbele kwa kupatiwa maeneo ya kufanyia biashara pindi majengo hayo yanapokamilika hivyo viongozi wa halmashauri wahakikishe wanatoa kipaumbele kwa wafanyabiashara waliokuwepo awali,” alisema Jafo.

Alisema kuwa Serikali imekuwa ikiwekeza katika miradi mikubwa ikidhani inawagusa maskini lakini kwa bahati mbaya masoko mengi yanayojengwa wanaonufaika ni watu wenye fedha na kuwaacha wafanyabiashara waliokuwepo awali kabla soko kujengwa.

Hivyo aliwaagiza Wakuu wa Wilaya kuhakikisha wananchi masikini wanapatiwa nafasi katika masoko hayo ili waweze kujiongezea kipato.

Pia alizitaka Halmashauri kuhakikisha kuwa kabla soko halijaanza kujengwa kufanyike tathmini ya wafanyabishara waliokuwepo awali ili wawe kipaumbele pale soko linapokamilika.

Wakati huohuo Mhe. Jafo amewataka wamachinga nchini kuhakikisha wanajiunga na bima iliyoboreshwa ili iwawezeshe kuwasaidia pale wanapokuwa wagonjwa wao na familia zao kwa kuwa afya ni uhai.

Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Bil 16.4/- zarejesha hadhi ya Shule za Sekondari za Ufundi nchini

    January 22, 2021
  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.