• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Book History
    • Kuhusu Wizara
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Utawala
    • Directory
    • Vitengo
    • Muundo wa Wizara
    • Mikoa, Wilaya na Halmashauri
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji

Serikali Kuendelea Kuimarisha Ukusanyaji wa Mapato ya halmashauri

Imewekwa tar.: February 26th, 2019

Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini zimetakiwa kuhakikisha kuwa fedha zote zinazokusanywa katika mapato zinawekwa benki kabla ya kupangiwa matumizi husika ili kuwa salama zaidi na kuhakikisha zinakwenda kutekeleza matumizi husika.

Hayo yamebainishwa na Katibu Mkuu Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (OR-TAMISEMI), Mhandisi Joseph Nyamhanga katika hafla ya upokeaji wa mashine za kielektroniki (point of sales machines) kutoka Serikali ya Dernmark ofisini kwake Jijini Dodoma leo.

“Makatibu Tawala wa Mikoa kuweni makini katika ukusanyaji wa mapato ili kutimiza azma ya serikali ya kuongeza udhibiti na kuleta tija katika ukusanyaji wa mapato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa kwa kuhakikisha fedha ilokusanywa inahifadhiwa benki kabla ya matumizi yoyote”Amesema Mhandisi Nyamhanga.

Aidha, Mhandisi Nyamhanga ameongeza kuwa jitihada hizi zinazofanywa na Serikali ya Awamu ya Tano zitasaidia kuongeza kipato katika Mamlaka za Serikali za Mitaa, kupunguza mianya ya izi wa fedha, kupunguza utegemezi na kuboresha utoaji wa huduma za kijamii kwa wananchi.

Naye Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt.Charles Muhina amesema kuwa hafla hiyo ya kukabidhi mashine hizo kwa mikoa hiyo ni mwendelezo wa kuziwezesha Halmashauri kuwafikia walipa kodi waliopo kwenye maeneo yao na kuongeza wigo katika ukusanyaji wa mapato katika maeneo yao.

“Sisi OR-TAMISEMI jukumu letu ni kufanya ufuatiliaji na tathimini ya utekelezaji wa mradi ili kuhakikisha kuwa mradi husika unatekelezwa kwa kuzingatia sheria, kanuni, na taratibu za nchi hii” Ameongezea Dkt. Muhina

Kwa upande wake Mkurugenzi wa TEHAMA Ofisi ya Rais TAMISEMI Erick Kitali ametoa wito kwa halmashauri kuwa na kifaa maalumu cha kuzuia radi ili kutatua changamoto ya mitandao ya mifumo ya mapato kaharibiwa radi kipindi cha mvua katika halmashauri hizo.

Awali Kiongozi wa Mradi Maboresho ya Mazingira ya Biashara Flemming Olsen ametoa wito kwa Serikali ya Jamhuri ya Muungano waTanzania kuhakikisha  mapato yanakusanywa kwa ufasaha kwani kuna wafanya biashara wanabidhaa ya thamani kubwa  lakini wanalipa ushuru mdogo.

Wakati huo huo Katibu Tawala wa Mkoa wa Kigoma Rashid Mchatta amesema kuwa atakwenda kusimamia vyema mashine hizo ili zifanye kazi ipasavyo na itasaidia kuongeza mapato katika maeneo yao ya kazi.

Katika hafla hiyo Mhandisi Nyamhanga amehitimisha kwa kutoa shukurni za dhati  kwa niaba ya Serikali ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania kwa wananchi wa Serikali ya Denmark kupitia Ubalozi wa Denmark nchini Tanzania na kusema kuwa ushirikiano wa nchi hizi mbili utaleta maendeleo kwa wananchi wa Tanzania kwa ujumla.

                                                          Anaandika Fred Kibano na Majid Abdulkarimu

Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 TANZANIA BARA December 06, 2019
  • TANGAZO LA KUWAREJESHA WAGOMBEA WASIO NA MAKOSA YA KIKANUNI KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019 November 10, 2019
  • MAELEZO KUHUSU ZOEZI LA KUCHUKUA NA KUREJESHA FOMU ZA MAOMBI YA UTEUZI WA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI October 30, 2019
  • TANGAZO NA ORODHA YA WALIOITWA AJIRA ZA MKATABA TAASISI YA BENJAMIN MKAPA October 25, 2019
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI KADA YA AFYA REPLACEMENT October 25, 2019
  • Orodha ya Majina ya watumishi wa Ajira Mpya kada ya Afya September 18, 2019
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Jafo atangaza waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza, 2020

    December 05, 2019
  • Jafo ambana Mkandarasi SKOIL Building Contractors Limited

    December 04, 2019
  • Jafo akagua ujenzi wa hospitali ya Uhuru

    December 04, 2019
  • Halmashauri zapigwa marufuku kukopa Benki

    November 29, 2019
  • Angalia zote

Video

Rais Dkt. John Pombe Magufuli Dodoma
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.