• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Nimeridhishwa na Uwekezaji wa Elimu Chato - Mweli

Imewekwa tar.: March 12th, 2020

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu Gerald Mweli amesema ameridhishwa na kutambua jitihada zinazofanywa na viongozi wa Wilaya ya Chato katika kuwekeza kwenye miundombinu ya Elimu.

Mweli ameyasema hayo wakati alipotembelea Wilaya hiyo na kukutana na Menejimenti, Walimu pamoja na kukagua ujenzi wa shule mbalimbali zilizoboreshwa na zinazoendelea kuboreshwa Wilayani hapo.

Mweli amesema  anatambua  jitihada kubwa  wanaazozifanya kwenye  eneo la Elimu, naona mmejiongeza kwa kuanzisha  kiwanda cha matofali ambayo yatatumika katika ujenzi wa madarasa hii ni jitihada nzuri sana katika kukuza sekta ya Elimu Wilayani Chato.

‘Naona mmeshafyatua matofali zaidi ya elfu tano na kazi inaendelea hii inanitia moyo; Kazi hii mnayoifanya itasaidia katika kupunguza gharama za ujenzi wa darasa hapa Chato kushuka kutoka Milioni 20 mpaka Milioni 10 kwa darasa moja kwahiyo kupitia mlango huu mtaweza kujenga madarasa ya kutosha’

Wilaya hii inawatoto wengi ambao wako shuleni na wengine wanakaribia kuanza shule hii inapelekea mahitaji makubwa ya vyumba vya madarasa ili watoto wote wenye umri wa kwenda shule wanaende na wapatiwe elimu bora aliongeza Mweli.

Katika kikao chake na Menejiment ya Halmashauri ya Wilaya Chato Mweli alisisitiza ukusanyaji wa mapato ya ndani ambayo kwa mwaka huu wa Fedha halmashauri hiyo inatakiwa kukusanya Bil 2.9 pia alipokea taarifa ya utoaji wa mikopo ya wanawake, vijana na walemavu.

Aidha wakati akizungumza na Walimu Mweli alitolea ufafanuzi wa masuala mbalimbali yaliyoibuliwa na kutokea ufafanuzi katika kupanda madaraja kuwa kigezo si muda tu bali ninutendaji kazi, namna ulivyopimwana kwenye Opras pamoja mahitaji ya nafasi hiyo kwa wakati husika.

‘Alisisitiza kuwa kupanda madaraja sio kufikisha muda tu kuna sifa nyingi za ziada zinazoangaliwa  kama hujazifikia zotr huwezi kupanda hata kama muda wako umefika hivyo tunatakiwa kujituma na kuleta matokeo katika maeneo yetu ya kazi wakati wote’  alisisitiza Mweli.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Chato Eliud Mwaiteleke amesema halmashauri hiyo imejipanga kikamilifu katika kuhakikisha inakuanya mapato ipasavyo na fedha hizo zinaenda kutekeleza miradi ya maendelea ikiwa ni pamoja na ujenzi wa vyumba vya madarasa.

Pia aliishukuru Serikali kwa kuwapatia vitendea kazi kama vile Mashine za kukusanyia mapato (POS) 43 ambazo kwa kiasi kikubwa zimedhibiti upotevu wa mapato.

‘Akitaja mikakati mingine waliyojiwekea katika ukusanyaji wa mapato Mwaiteleke amesema ni kuanzisha kiwanda  cha kufyatua matofali ambacho kimeshaanza kufanya kazi,  ofisi ya kurudisha (Printing Unit) pamoja ufugaji.

Katika utoaji wa Mikopo ya vikundi vya wanawake, vijana na watu wenye ulemavu Mwaiteleke amesema wamefungua akaunti maalumu ya Mikopo hiyo kwa mujibu wa maelekezo na kwa mwaka wa fedha uliopita mikopo iliyotolewa ni shilingi mil 117 sawa na asilimia 87 ya malengo waliyojiwekea.

‘Kwa mwaka huu wa fedha mikopo iliyotolewa katika robo ya kwanza ni shiling mil 51 zaidi ya lengo la kutoa Mil 50  iliyowekwa na kutoka Ofisi ya Waziri Mkuu walitoa shilingi Mil 78 kwa ajili ya mikopo kwa vikundi vingine ‘ aliongeza Mwaiteleke.

Mahitaji ya Ujenzi wa vyumba vya madarasa katika Halmashauri ya Wilaya ya Chato ni 2257 kwa shule za Msingi na Sekondari na hii kutokana na idadi kubwa ya wanafunzi waliopo katika Wilaya hiyo.

Naibu Katibu Mkuu Mweli akiwa Chato alitembelea kiwanda cha halmashauri cha kufyatua matofali mfungamano (Interlock) shule ya Msingi Chato na Magufuli, shule ya sekondari Magufuli pamoja na Buselesele.

Nteghenjwa Hosseah, Chato


Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Bil 16.4/- zarejesha hadhi ya Shule za Sekondari za Ufundi nchini

    January 22, 2021
  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.