• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Kuhusu Sisi
    • Book History
    • Kuhusu Wizara
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
  • Utawala
    • Directory
    • Vitengo
    • Muundo wa Wizara
    • Mikoa, Wilaya na Halmashauri
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Bajeti na Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji

Nimeridhishwa na usimamizi wa ujenzi wa vituo vya afya nchini

Imewekwa tar.: April 4th, 2019

Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Joseph Pombe Magufuli ameipongeza Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kwa kushirikiana na Wizara ya afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto kwa usimamizi  wenye weledi  katika ujenzi na ukarabati wa vituo vya kutolea huduma za Afya Nchini.

Ameyasema hayo leo kwenye uzinduzi wa Kituo cha Afya cha Mbonde katika Halmashauri Mji wa Masasi, Mkoani Mtwara kwa niaba ya vituo 352 vya kutolea huduma nchini ambavyo vimejengwa katika Halmashauri zote nchini.

Mhe. Magufuli amesema kuwa Serikali imetenga fedha kwa ajili ya ujenzi wa vituo vya kutolea huduma lakini Wizara hizo mbili zimeweza kusimamia kwa weledi utekelezaji wa ujenzi wa vituo hivyo.

“Kutengwa kwa fedha ni sula la msingi lakini usimamizi wa fedha ni suala muhimu sana hivyo  nimeridhishwa na usimamizi uliofanywa na Wizara hizi mbili  ambapo ujenzi umefanyika kwa kiwango kikubwa na  usimamizi huo unaacha alama kwa nchi na kupunguza kero za miundominu ya afya nchini” Amesema Mhe. Magufuli

Mhe. Magufuli amewapongeza watumishi wa  OR-TAMISEMI  na Wizara ya Afya kwa kujitoa kwa hali na mali katika kusimamia na kuhakikisha vituo vya afya vinakamilika kwa wakati na viwango vya juu na kuanza kutoa huduma kwa jamii ili kuwahudumia wananchi maskini nchini.

 “Panapostahili kupongezwa napongeza hadharani bila kificho na sitasubiri mpaka mtu afe, kwa kweli Wizara hizi mbili wamesimamia kazi ya ujenzi wa vituo vya afya kwa umakini mkubwa na wamefanyakazi nzuri” Amesisitiza Mhe. Magufuli

Amesema kuwa kwa gharama ya shilingi milioni 500 wameweza kujenga Wodi ya Wazazi, Jengo la Maabara, Chumba cha kuifadhia maiti,  chumba cha Mionzi na Jengo la upasuaji hivyo nimeridhishwa na matumizi ya fedha zilizotolewa na Serikali na wadau wa maendeleo katika Sekta ya afya

Mhe. Magufuli amewapongeza Wataalam wa afya nchini  kwa kufanyakazi kwa weledi na moyo wa kujitolea na kuwataka  kuendelea kutoa huduma bora kwa jamii maskini ambao ndio wenye uhitaji mkubwa wa huduma za afya nchini.

Aidha Mhe. Magufuli amefafanua kuwa gharama zilizotumika katika ujenzi wa vituo 352 ni shilingi bilioni 184 hivyo amewashukuru wananchi, wadau wa maendeleo kwa kujitoa kwa moyo  kuleta maendeleo katika Sekta ya afya nchini.

Wakati Huohuo Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo amesema kuwa sekta ya afya ni eneo linalogusa wananchi wa hali ya nchini hivyo serikali iliamua kuwekeza katika sekta ya afya ili kuleta mabadiliko katika jamii.

Amesema tangu uhuru kulikuwa na Hospitali za Serikali 77 katika Halmashauri 185,  vituo vya afya 535 ambapo viliyokuwa na uwezo wa kufanya upasuaji ni  vituo vya afya 118  hali hii ilikuwa ikisababisha vifo vya mama na mtoto pale anapohitaji kujifungua kwa njia ya upasiaji kwa kuwa walikuwa wakitembea muda mrefu kufuata huduma hizo katika Hospitali za Rufaa.

Aidha Mhe Jafo amesema katika miezi 18 ya ujenzi wa vituo vya afya nchini Serikali imeweza kufanya mapinduzi makubwa katika sekta ya afya ambapo mpaka sasa vituo 352 vimeweza kujengwa na vinaweza kufanya huduma ya upasuaji.



Matangazo

  • UCHAGUZI WA WANAFUNZI WA KUJIUNGA NA KIDATO CHA KWANZA MWAKA 2020 TANZANIA BARA December 06, 2019
  • TANGAZO LA KUWAREJESHA WAGOMBEA WASIO NA MAKOSA YA KIKANUNI KWENYE UCHAGUZI WA SERIKALI ZA MITAA 2019 November 10, 2019
  • MAELEZO KUHUSU ZOEZI LA KUCHUKUA NA KUREJESHA FOMU ZA MAOMBI YA UTEUZI WA KUGOMBEA NAFASI ZA UONGOZI October 30, 2019
  • TANGAZO NA ORODHA YA WALIOITWA AJIRA ZA MKATABA TAASISI YA BENJAMIN MKAPA October 25, 2019
  • TANGAZO LA KUITWA KAZINI KADA YA AFYA REPLACEMENT October 25, 2019
  • Orodha ya Majina ya watumishi wa Ajira Mpya kada ya Afya September 18, 2019
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Jafo atangaza waliochaguliwa kujiunga na Kidato cha kwanza, 2020

    December 05, 2019
  • Jafo ambana Mkandarasi SKOIL Building Contractors Limited

    December 04, 2019
  • Jafo akagua ujenzi wa hospitali ya Uhuru

    December 04, 2019
  • Halmashauri zapigwa marufuku kukopa Benki

    November 29, 2019
  • Angalia zote

Video

Rais Dkt. John Pombe Magufuli Dodoma
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.