• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App

Naibu Katibu Mkuu ahimiza Ushirikiano katika kazi

Imewekwa tar.: May 3rd, 2018

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia Elimu bwana Tixon Nzunda amewaasa watumishi wa ofisi hiyo kufanya kazi kwa bidii na kwa weledi ili waweze kutimiza malengo waliyojiwekea ya kutoa huduma kwa wananchi kwa ufanisi zaidi.

Akizungumza wakati wa kikao cha baraza la wafanyakazi kilichofanyika jana katika ukumbi wa Chuo cha Serikali za Mitaa Hombolo, nje kidogo ya jiji la Dodoma, Bwana Nzunda alisema kuwa kutokana na Ofisi hiyo kupewa majukumu makubwa ya kiutendaji, watumishi wana wajibu wa kufanya kazi kwa kushirikiana katika kujenga umoja wa ofisi hiyo.

Alisema kuwa watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI wanapaswa kuzingatia maadili na misingi ya utoaji huduma bora na kujiepusha na vitendo vya rushwa na wakumbuke kuwa Ofisi hiyo ipo chini ya Mheshimiwa Rais, na hivyo wanajukumu la kumwakilisha Rais vizuri katika utoaji wao huduma kwa wananchi.

Pia aliwashauri watumishi hao kujiepusha na vitendo vitakavyopelekea kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi (VVU) na magonjwa mengine sugu na pia aliwahimiza kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ili kuwa na afya njema itakayowawezesha kufanya kazi zao vizuri.

Wakati huo huo Naibu Katibu Mkuu amewapongeza wafanyakazi bora wa Ofisi ya Rais TAMISEMI waliochaguliwa kwa mwaka 2018, ambapo pia aliagiza wafanyakazi hao wapewe zawadi zao bila kucheleweshwa ifikapo kesho.

Pia alimpongeza Katibu Mkuu Ofisi ya Rais TAMISEMI Mhandisi Mussa Iyombe kwa maelekezo yake yaliyofanikisha kazi kubwa ya kuandaa bajeti ya Ofisi ya Rais TAMISEMI mwaka 2018.

Mapema Kaimu Mkurugenzi wa Utawala na Raslimali watu bwana Mrisho Mrisho alimweleza Naibu Katibu Mkuu na wajumbe wa baraza la wafanyakazi kuwa kutokana na Ofisi ya Rais TAMISEMI kuongezewa majukumu ya utendaji kazi, idadi ya watumishi katika ofisi hiyo imeongezeka na kufikia watumishi 678 hivi sasa.

Alisema kuwa idadi hiyo imejumuisha watumishi kutoka Wakala wa Barabara Vijijini na Mijini (TARURA) na watumishi wengine wanaokuja kuimarisha idara mbalimbali za TAMISEMI.

Kwa upande wake Mwenyekiti wa chama cha Wafanyakazi wa Serikali na Afya (TUGHE)  Mkoa wa Dodoma bwana John Mchenya aliwataka viongozi wa tawi la Tughe kutoka Ofisi hiyo kufanya vikao vya mara kwa mara na watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI  ili wahamasike kujiunga na chama hicho.

Bwana Mchenya alisema kuwa yeye binafsi atakuwa mstari wa mbele kushiriki katika vikao hivyo ili waweze kuwahamasisha watumishi wengi wanaofanya kazi TAMISEMI ambao wametoka kwenye Mamlaka za Serikali za Mitaa kujiunga na chama hicho.

Anaandika Methew Kwembe OR-TAMISEMI

Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Natoa siku siku 12 mtatue kero za soko la Ndugai na Stendi kuu ya Mabasi- Waziri Jafo

    March 03, 2021
  • Agizo la ujenzi wa vyumba vya madarasa 2257 latekelezwa

    March 02, 2021
  • Waziri Jafo ataka Shilingi Bilioni 245 za Miradi ya Maendeleo zitumike kwa wakati

    March 01, 2021
  • Serikali yalegeza masharti mikopo ya asilimia 10

    February 27, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.