• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

Imewekwa tar.: January 11th, 2021

Na Atley  Kuni, Shinyanga

Naibu Katibu Mkuu, Ofisi ya Rais - TAMISEMI, (anayeshughulikia elimu), Bw. Gerald Mweli, amesema Wanafunzi wa kidato cha Nne na Sita, muda wao walionao kwa sasa ni miezi Minne kwa kidato cha Sita na Miezi tisa kwa kidato cha Nne kuamua hatma ya maisha yao kielimu na mafanikio yao kimaisha. Bw. Mweli aliyazungumza hayo wakati wa ziara yake ya kikazi leo tarehe 11 Januari, 2021 mkoani Shinyanga

“Muda mlionao ninyi ni mchache sana wa kuamua hatma ya maisha yenu kielimu, kuna wenzenu walifukuzwa shule huko mkoani Arusha juma moja kabla ya kuanza mitihani yao ya kuhitimu baada ya nidhamu yao kwenda kinyume na sheria, taratibu na kanuni za shule kwa kuharibu miundombinu ya shule.” alisema Mweli na kuzidi kusisitiza kuwa Uvutaji bangi, uzinzi, upigaji mawe na kuharibu miundombinu ya shule ni baadhi ya makosa ambayo yataweza kuwafukuzisha shule hata kama wamebakiza siku mbili kuanza mitihani yao, hivyo akawaasa wawe wanafunzi watiifu.

Mweli amewaonya wanafunzi hao kuwa, endapo watashindwa kuzingatia nidhamu wakiwa shuleni hapo, basi ipo siku watafunzwa nidhamu wakiwa chini ya miongozo ya vyombo vya dola vya polisi na Magereza, “Sitaki kuona vijana wangu, wadogo zangu mnafikia huko.

“Kidato cha sita tambueni mna miezi minne tu ya kuamua hatma yenu, na ninyi kidato cha Nne mna miezi Tisa tu, hivyo ni hiyari yenu kuamua nini mnakihitaji katika Maisha yenu siku zijazo, ni wazi kwamba, kusoma sio kibali cha kutajirika, lakini itakusadia na kukujengea heshima mbele ya jamii yako.” Mweli amewasisitiza wanafunzi hao.

Awali akitoa taarifa ya Shule ya Sekondari Shinyanga, mbele ya Naibu Katibu Mkuu, Mkuu wa Shule hiyo Benard Ishengoma, amemwambia Naibu Katibu Mkuu kuwa, Shule ya Sekondari Shinyanga ilipokea kiasi cha Shilingi 897,335,247.05 kwa ajili ya ukarabati wa shule hiyo kongwe yenye zaidi ya miaka 55 toka kuanzishwa kwake mnamo mwaka 1966.

Akiwa shuleni hapo, Naibu Katibu Mkuu, amewakumbusha walimu majukumu yao lakini pia, kuwataka kuwasimamia wanafunzi na kuwahimiza kujiunga na Klabu mbalimbali ikiwepo Skauti, lakini pia kuwakumbusha kuzingatia suala la uzalendo ikiwepo kuwafundisha wanafunzi nyimbo za kizalendo ikiwepo, Wimbo wa Taifa, Wimbo wa Afrika Mashariki sambamba na Wimbo wa Uzalendo wa Tanzania nakupenda kwa moyo wote, kila mara.

Naibu Katibu Mkuu Gerald mweli amefika shuleni hapo ikiwa ni sehemu ya ziara yake, ambapo katika siku ya kwanza mbali ya kutembelea shule ya Sekondari Shinyanga ametembelea na kukagua Shule ya msingi Buhangija, Shule ya Sekondari Mwadui ufundi na Shule ya Sekondari Maganzo na kisha kufanya mkutano wa pamoja na Waratibu Elimu Kata, Wakuu wa Shule na Walimu Wakuu.

MWISHO

Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Vikundi 47 Kondoa vyapewa mikopo ya shilingi milioni 147

    February 24, 2021
  • Mikopo ya Shilingi Milioni 85 yatolewa kwa Vikundi wilayani Bunda

    February 24, 2021
  • Mradi wa Fursa na Vikwazo Iliyoboreshwa Kuingizwa kwenye Majukumu ya OR - TAMISEMI

    February 23, 2021
  • Mikopo ya Sh. Milioni 850 yatolewa kwa Vikundi 104 jijini Tanga

    February 15, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.