• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu

Matumizi ya tofali za mfungamano katika ujenzi wa madarasa wamfurahisha Naibu Katibu Mkuu

Imewekwa tar.: March 13th, 2020

Na Nteghenjwa Hoseah, Geita

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa TAMISEMI anayeshughulika Elimu Gerald Mweli amefurahishwa na ubunifu wa kutumia tofali mfungamano (Interlock) kwenye ujenzi wa vyumba vya madarasa katika kukabiliana na mrundikano wa wanafunzi katika shule za  Mkoa wa Geita.

Mweli ameonyesha furaha yake wakati wa ziara ya kikazi Mkoani humo iliyokua na lengo la kukagua miundombinu ya Elimu iliyojengwa na inayoendelea kujengwa pamoja na  kupokea changamoto za walimu na kuzitolea ufafanuzi.

Akiwa Mkoani Geita Mweli aliweza kujionea namna ambavyo Mkoa huo umejiongeza kwa kupeleka mashine za kufyatulia matofali mfungamano katika Halmashauri zote na kujenga darasa la mfano kwa kutumia tofali hizo katika shule ya sekondari nyanza.

Akikagua darasa hilo Mweli amesema ubunifu ni wa kuigwa na Mikoa mingine sababu umeonyesha umakini wa hali ya juu wa viongozi wa Mkoa wa Geita, uzalendo, kujitoa  na kupunguza changamoto ya uhaba wavyumba vya  madarasa katika shule za Serikali.

“Nimefarijika sana kuona darasa limekamilika kwa kutumia matofali haya ambayo ni ya gharama nafuu kwani sasa gharama za ujenzi wa chumba cha darasa kwa mkoa wa Geita imeshuka kutoka shilingi milioni 20 mpaka kufikia milioni 11 tu hili ni jambo zuri na la mfano nawapogeza sana Geita” alisema Mweli.

Mweli aliongeza kuwa Geita ni miongoni mwa mikoa yenye uhaba mkubwa wa vyumba vya madarasa na shule zake nyingi zina wanafunzi wengi mno kiasi kwamba hata ufundishaji wa wanafunzi hao inakuwa changamoto  lakini viongozi wa mkoa huu wamejiongeza na kuja na ubunifu huu wa kupunguza gharama za ujenzi kwa kutumia matofali mfungamano na kwa mpango huu tutaweza kujenga vyumba vingi zaidi na kupunguza changamoto ya mlundikano wa wanafunzi.

Akizungumzia mpango huo Mkuu wa Mkoa wa Geita Mhe. Robert Gabriel amesema wao kama viongozi hawataki mpaka waagize kutoka juu wanabainisha changamoto walizonazo, wanaweka mikakati mapema, na kuanza kutekeleza kwa wakati na kutatuza changamoto zao.

“Mahitaji ya vyumba madarasa katika Mkoa wetu ni zadi ya vyumba 9000 na tunategemea wanafunzi wengine watamaliza shule hivi karibuni hivyo mahitaji yataongezeka zaidi ya sasa tunajiandaa mapema kukabiliana na mahitaji tuliyonayo” alisema Mhe. Robert Gabriel.

Aliongeza kuwa mashine hizi za kufyatulia matofali ya mfungamano zilikuwepo tangu zamani lakini hazikuwa zikitumika, nikaona ni muda sasa kuzigawa kwa kila halmashauri kuwaelekeza namna ya kuzitumia ili nao waanze kufyatua matofali ya kujengea madarasa: Kwa hapa Geita tumeshajenga darasa moja la mfano katika shule ya Sekondari Nyanza kwa kutumia tofali hizi na tumelikamilisha kabisa kwa kutumia gharama ya shilingi Mil 11 tu hivyo watu wote nawakaribisha waje hapa wajionee darasa hili.

Naye Mkurugenzi wa usimamizi wa Elimu OR-TAMISEMI Julius Nestory wakati wa kikao na waratibu wa elimu Kata, wakuu wa shule pamoja na walimu wakuu aliwakumbusha wataalamu hao kuwa sifa za kuwa kiongozi wa Elimu ni lazima uwe na uwezo wa kuwasimamia walio chini yako, kufanya maamuzi na kuyasimamia na kuhakikisha kuwa unaishi karibu na eneo lako la kazi.

Mkurugenzi Nestory aliwakumbusha Waratibu wa Elimu kata kuwa ni lazima wawe na barua za utezi wa nafasi hiyo, wawe na shahada husika na wakae kwenye kata aliyopangiwa na si vinginevyo.

Naibu Katibu Mkuu Mweli akiwa katika Mkoa wa Geita alitembelea shule ya sekondari nyanza, kalangalala shule ya msingi pamoja na shule ya mchepuo wa Kingereza ya bombambili.


Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Waziri Jafo ataka Zimamoto, Skauti wakomeshe majanga ya moto shuleni

    February 26, 2021
  • Vikundi 13 Wilayani Kibaha vyanufaika na mikopo ya sh milioni 46

    February 25, 2021
  • Magufuli: Viongozi tatueni kero za wananchi kwa wakati

    February 25, 2021
  • Shilingi Bilioni 3 zakwamua Wanawake, Vijana na Walemavu Geita

    February 25, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.