• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu

Mamlaka za Serikali za Mitaa zatakiwa kuweka agenda ya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza.

Imewekwa tar.: November 12th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI) Mhe. Selemani Jafo amezielekeza Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kila kituo cha afya nchini kinaweka ajenda ya kudumu ya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza ili kuwasaidia wananchi wenye matatizo ya kiafya katika Mamlaka hizo.

Mhe.Jafo amesema hayo leo kwenye uzinduzi wa upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza yanayofanyika katika viwanja vya Jamhuri Jijini Dodoma wakati wa maadhimisho ya kitaifa ya wiki ya kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukiza nchini.

“Wakurugenzi wa Halmashauri na Waganga Wakuu hakikisheni mnasimamia ajenda hii kwa weledi mkubwa ili kuimarisha afya za watanzania kwa lengo la kuinua uchumi wa taifa letu kwani bila afya bora watu hawataweza kufanya kazi kwa ubora unaotakiwa.” amesisitiza Mhe.Jafo

Mhe.Jafo amesema kuwa ni vyema kuanzisha kiliniki maalumu kwa ajili ya upimaji wa magonjwa yasiyoambukiza katika Halmashauri ili kusaidia kubaini watu wenye magonjwa hayo kwa haraka na kuweza kupatiwa tiba sahihi.

“Kiliniki hizi zitasaidia watanzania kuweza kupata ushauri wa afya zao, upimaji wa afya na tiba juu ya magonjwa haya yasiyoambukiza lengo ikiwa ni kujenga utamaduni kwa watu kwenda wenyewe kupima kwa hiari bila kulazimishwa” ameeleza Mhe. Jafo

Mhe. Jafo ametoa rai kwa wananchi  wote  kufanya mazoezi , kula vyakula kama matunda, mbogamboga na kujiepusha na matuzi ya vyakula  vyenye wanga mwingi, sukari, chumvi na mafuta ili kujiepusha na magonjwa yasiyoyakuambukiza na  kuimarisha nguvu kazi ya taifa .

Naye Mkuu Mkuu wa Wilaya Dodoma Bw. Patrobas Katambi amewataka wananchi kujenga utamaduni wa kufanya mazoezi ili kulinda afya zao na kuepuka magonjwa yasiyoambikiza.

Wakati huohuo, Kaimu Mkurugenzi wa Magonjwa yasiyoambukiza Dkt. Sarah Maongezi amesema maadhimisho hayo yataenda sambamba na upimaji wa afya, ushauri wa afya kutoka kwa wataalam wa afya,  matamasha ya michezo na kongamano la kisayansi litakalojadili magonjwa yasiyoambukiza litakalofanyika 12-13 Novemba , 2019 na kuzindua mpango wa kuzuia na kupambana na magonjwa yasiyoambukiza.

Aidha, kauli mbiu ya maadhimisho hayo ni “Tutembee pamoja katika kuzuia na kudhibiti magonjwa yasiyoambukizwa” lengo likiwa ni kuhimiza ushirikiano katika kudhibiti magonjwa haya kwani mapambano dhidi ya vihatarishi vya magonjwa yasiyoambukiza yanahusisha mshikamano wa sekta mbali mbali, wadau, mtu mmoja mmoja na wananchi kwa ujumla.





Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Vikundi 23 Wilayani Busega vimenufaika na mikopo ya asilimia 10

    February 26, 2021
  • Vikundi 366 Wilayani Kilwa vyanufaika na mikopo ya sh bilioni 1.1

    February 26, 2021
  • Waziri Jafo ataka Zimamoto, Skauti wakomeshe majanga ya moto shuleni

    February 26, 2021
  • Vikundi 13 Wilayani Kibaha vyanufaika na mikopo ya sh milioni 46

    February 25, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.