• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Madiwani kuanza kupimwa kwa kuwawezesha Wanawake Kiuchumi

Imewekwa tar.: July 30th, 2019

Makamu wa Rais wa jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Samia Suluhu Hassan amewataka Madiwani wa Halmashauri zote Nchini kutumia muda wao mwingi kukomesha vitendo vya unyanyasaji wa  Wanawake na watoto katika maeneo ya masoko na mikusanyiko  sambamba na kuwezesha kundi hilo kuweza  kujikwamua kiuchumi.

Mhe.Samia ameyasema hayo wakati akizindua mradi wa kutokomeza vitendo vya unyanyasaji na udhalilishaji dhidi ya Wanawake na Watoto kwenye maeneo ya masoko unaotekelezwa katika Manispaa za Dodoma na Shinyanga.

“Ifike wakati sasa Waheshimiwa Madiwani waanze kupimwa kutokana na namna walivyoweza kuwakwamua wanawake na watoto kutoka katika hali ya kunyanyaswa na wawezeshe kundi hulo kujikwamua kiuchumi kuwa na maendeleo endelevu” alisema Mhe. Samia.

“Madiwani watusaidie kutoa elimu ya athari za unyanyasi wa kijinsia kwa jamii na wanawake hawa wajengewe uwezo wa namna ya kuunda vikundi vyenye manufaa na hao hao madiwani wahakikishe wanapatiwa mikopo yenye Tija kwa ajili ya kuendeleza biashara zao na kipato kwa ujumla” Aliongeza Mhe.Samia.

Sambamba na hilo Mhe. Samia alisema katika kupambana na vitendo hivyo vya kikatili na unyanyasaji wa Wanawake  Serikali imeimarisha utendaji wa madawati 417 ya jinsia yaliyopo katika vituo vya Polisi kote nchini kwa lengo la kuwezesha huduma stahiki kwa watu wanaofanyiwa ukatili wa kijinsia.

Aidha Mhe. Samia ameitaka Wizara ya Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto pamoja na Ofisi ya Rais-TAMISEMI kushirikiana na Jumuiya ya Tawala za Mitaa Tanzania (ALAT) ambao ndio waratibu wa mradi huu katika kuhakikisha afua zinazotekelezwa kupitia mradi huo zinakua endelevu hata pale utekelezaji wa mradi unapofikia mwisho.

"Ndugu zangu kila mmoja wetu ana haki ya kupinga na kutokomeza ukatili wa kijinsia, hivi vitendo havikubaliki na wala haviruhusiwi kisheria. Yeyote atakayethubutu kumdhalilisha mwanamke au mtoto tutamchukulia hatua kali.

"Ni jambo la aibu kuona tunatumia viungo vya wanawake kama matusi, huyu mwanamke unayemdhalilisha tukumbuke ni kama mama zetu majumbani mwetu, hatuwezi kuwa na Taifa lenye amani kama tutaruhusu vitendo hivi, tuungane katika kupiga vita na kutokomeza ukatili wa kijinsia, " amesema Mhe. Samia.

Akizungumzia wimbi la watoto wadogo kufanya biashara kwenye masoko, Mhe. Samia amezitaka kamati za masoko kuhakikisha zinashirikiana na mamlaka husika katika kuzuia watoto kufanya biashara sokoni na badala yake wawahimize kwenda shule na kuwaripoti wazazi wanaowatuma watoto wao kufanya biashara.

"Serikali yenu ya awamu ya tano iliwaahidi elimu bure kwa shule ya msingi hadi kidato cha nne. Tunapoona watoto wetu hawaendi shule na wanafanya biashara sokoni tunakua hatumtendei haki Rais wetu Dk John Magufuli kwa zawadi ya elimu bure aliyotuletea. Tuwazuie watoto kufanya biashara sokoni na tushirikiane kuwapeleka shule," amesema Mhe. Samia.

Aidha katika kutekeleza mradi huo, Makamu wa Rais Mhe.Samia Suluhu Hassan amekabidhi Pikipiki 14 kwa ajili ya wataalam wa Maendeleo ya Jamii wa Mkoa wa Dodoma kwa Kata za Halmashauri ya Chamwino na kuielekeza Wizara kuendeleza utaratibu huo wa kupatia wataalamu hao usafiri ili iwe rahisi kwao kuwafikia wanawake wengi hususani wa vijijini na kuwaunganisha na fursa za kiuchumi.

Kwa upande wake Naibu Waziri Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Josephat Kandege amesema hivi sasa  katika Halmashauri utoaji wa Mikopo kwa Wanawake, Vijana na Walemavu inatolewa kwa mujibu kisheria hivyo itatolewa ipasavyo nakuongeza uwezo wa kundi hili kufanya biashara zenye tija.

“Wanawake watakapowewa mikopo ya uhakika itawawezesha  kujiongezea kipato ambapo kwa namna moja ama nyingine itasaidia kupunguza unyanyasaji na ukatili kuanzia katika ngazi ya familia kwa kuwa sasa kutakua na kipato cha uhakika” alisema Mhe. Kandege.

Naye Waziri wa Afya, Maendeleo ya Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, Mhe Ummy Mwalimu amemshukuru Makamu wa Rais kwa kuzindua mradi huo ambao utakua msaada mkubwa katika mapambano dhidi ya ukatili wa kijinsia.

"Mhe Makamu wa Rais kama Wizara tumejipanga katika kuhakikisha tunaongeza elimu zaidi kwa wananchi iki tuzidi kupunguza wimbi la vitendo hivi, lengo letu ni kutokomeza kabisa vitendo hivi ili kuwa na Taifa imara ambalo litakua na mshikamano na amani baina yetu bila kujali huyu ni Mwanaume au Mwanamke," amesema Waziri Ummy.

.

Naye Mwenyekiti wa ALAT Mhe, Gulamhafeez Mukadam amesema kuna changamoto kwenye dira ya pamoja juu ya utokomezaji wa vitendo vya ukatili wa kijinsia jambo ambalo linaleta athari ya maendeleo ya wanawake na hivyo kuzorotesha uchumi wa Nchi.

"Nimpongeze Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma, Mhe Godwin Kunambi kwa namna ambavyo amekua msaada kwa akina Mama wa Jiji hili kwa kuwapatia mikopo inayowawezesha kufanya biashara zao. Serikali za Mitaa jukumu lao ni kuwawezesha wananchi wao kuzipata fursa.

"Lakini pia kuna changamoto ya masoko, lugha chafu kwa wanawake sokoni hizi changamoto zinapaswa kushughulikiwa na kutokomezwa kabisa. Tukiwawezesha wanawake na kuwaepusha na vitendo vya unyanyasaji tutakua tunatengeneza Taifa imara na madhubuti na kuweza kufikia azma ya Mhe Rais ya uchumi wa kati kupitia viwanda," amesema Mhe Mukadam.

Beatrice Yame ni mwakilishi wa wanawake wafanyabiashara katika masoko ya Dodoma akizungumza wakati wa uzinduzi huo amesema watafurahia kuona haki inatendeka masokoni na uhusiano wa kijinsia unaimarishwa ili waweze kufanya biashara zao kwa amani na utulivu.

Mwisho.


Matangazo

  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Taarifa ya ukusanyaji wa mapato ya ndani ya Halmashauri kwa kipindi cha nusu Mwaka (Julai – Disemba, 2019) kwa Mwaka wa fedha 2019/2020 February 09, 2020
  • Tangazo la kazi kada ya Afya January 20, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • “PS3 plus” Yarudi kwa kishindo, Bilioni 114 kuwezesha Mifumo Sekta ya umma nchini

    January 16, 2021
  • Serikali yagawa vifaa vya bilioni 3 kwa Wanafunzi 18,488 wenye mahitaji maalum

    January 14, 2021
  • Mweli awatolea uvivu kidato cha Nne, Sita, awajenga kinidhamu

    January 11, 2021
  • Mweli awatega Wakuu wa Shule, Walimu Wakuu kwenye Mfumo wa PREM/PREMS.

    January 10, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.