• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App

Maafisa Manunuzi na Wakaguzi wa ndani kutoka halmashauri 118 wapigwa msasa

Imewekwa tar.: February 11th, 2019

Jumla ya watumishi 280 ambao ni Maafisa Manunuzi na Wakaguzi wa Ndani kutoka Halmashauri 118 za Mikoa 16 nchini wanashiriki mafunzo ya siku nne yanayofanyika mkoani Morogoro kwa lengo la kuwajengea uwezo maafisa hao ili waweze kuutumia vizuri Mfumo wa utoaji wa taarifa za ununuzi pamoja na marekebisho ya Sheria ya Ununuzi wa Umma ya mwaka 2016 pamoja na marekebisho ya kanuni zake.

Mafunzo hayo yanaendeshwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kupitia Programu ya Maboresho ya Fedha za Umma Awamu ya V (PFRMP V) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) ambao ndiyo wawezeshaji kwenye mafunzo hayo.

Akifungua mafunzo hayo jana mjini Morogoro, Katibu Tawala wa Mkoa wa Morogoro bwana Clifford Tandari alisema kuwa baada ya serikali kuifanyia marekebisho kadhaa sheria ya manunuzi ya umma kulikuwa na umuhimu mkubwa kwa watendaji hao kujengewa uwezo ili waweze kutekeleza majukumu yao kwa ufanisi.


Aliongeza kuwa Serikali iliona kulikuwa na haja ya kuifanyia marekebisho sheria hiyo ili iweze kuleta matokeo yaliyokusudiwa hasa kufanikisha lengo la upatikanaji wa thamani halisi ya fedha katika manunuzi kama ilivyokuwa imekusudiwa.
Kwa mujibu wa Katibu Tawala huyo, baadhi ya changamoto zilizokuwa zikiikabili sekta ya Ununuzina kupelekea Sheria na Kanuni hizo kurekebishwa ni pamoja na bei ya manunuzi kuwa kubwa kulinganisha na bei ya soko, gharama za mchakato wa manunuzi kuwa juu kutokana na mpangilio mbaya wa ununuzi na pia kutozingatia sheria, kanuni na miongozo inayotolewa na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA.
Bwana Tandari alizitaja changamoto nyingine kuwa ni pamoja na mchakato wa ununuzi kuchukua muda mrefu jambo ambalo limekuwa likileta athari mbalimbali ikiwemo kupanda kwa bei ya huduma, vifaa au kandarasi kutokana na hali ya soko kubadilika.
Changamto nyingine ni kutotumiwa kwa viwango hasa kwenye huduma na bidhaa kama vile utengenezaji wa magari, ununuzi wa bidhaa mtambuka hasa bidhaa zinazopatikana GPSA na MSD kwani lazima bidhaa hizo zitoke huko.
Bwana Tandari alieleza pia tofauti kati ya taratibu za ununuzi zinazotumiwa na Halmashauri na Taasisi nyingine za Umma hasa kutokana na kukosekana kwa taratibu za kisheria zinazowahakikishia wauzaji kuwa ununuzi unazingatia ushindani thabiti, haki, uwazi na uwajibikani, uadilifu na maslahi ya taifa.

Katibu Tawala wa Mkoa aliongeza kuwa kutokana na marekebisho ya sheria ya ununuzi serikali inatarajia kuongezeka kwa ushindani na uwazi katika ununuzi wa uma, kuongezeka kwa uwajibikaji na kupungua kwa gharama za ununuzi wa magari kwa kupitia Wakala wa Huduma ya Ununuzi Serikalini na kuboresha ukidhi na uzingatiaji wa sheria ya ununuzi ambapo sheria imetoa fursa kwa PPRA kuzikagua taasisi nunuzi na kupima kama zimezingatia ukidhi wa sheria katika ununuzi.
Bwana Tandari alisema kuwa sheria imetoa mwanya pia wa kutumia mfumo wa TEHAMA  ambapo taasisi nunuzi huwasilisha taarifa zake PPRA kwa kutumia mifumo iliyowekwa.
Kwa upande wake Mratibu wa Mafunzo hayo bwana Lucas Mrema alisema kuwa mikoa 16 inayoshiriki mafunzo haya ni  mbali na ile mikoa 10 iliyokuwa ilishiriki kwenye utekelezaji wa programu ya usimamizi wa fedha za Umma awamu ya nne.
" Katika utekelezaji wa programu ya Usimamizi wa Matumizi ya fedha za Umma awamu ya tano tunatarajia kuwa mikoa yote 26 na halmashauri zake 185 zitashirikishwa," alisema.
Kwa upande wake Mhandisi Mary Swai Kaimu Mkurugenzi Msaidizi kutoka Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA) aliwataka Maafisa Manunuzi kuhakikisha kuwa wanafuata taratibu zote za manunuzi pindi wanapotekeleza najukumu yao.
Aliongeza kuwa Maafisa Manunuzi wanapaswa kuhakikisha kuwa makini katika utekelezaji wa mikataba mbalimbali ambapo alidai kuwa pindi mkataba unaposainiwa wahakikishe kuwa mkataba huo unatekelezwa vizuri.
Anaandika Mathew Kwembe, Morogoro

Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Uhaba wa Saruji wachelewesha ujenzi wa barabara za Mji wa Serikali

    March 03, 2021
  • Natoa siku siku 12 mtatue kero za soko la Ndugai na Stendi kuu ya Mabasi- Waziri Jafo

    March 03, 2021
  • Agizo la ujenzi wa vyumba vya madarasa 2257 latekelezwa

    March 02, 2021
  • Waziri Jafo ataka Shilingi Bilioni 245 za Miradi ya Maendeleo zitumike kwa wakati

    March 01, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.