• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

JAFO: Jengeni mahusiano mazuri mahala pa kazi

Imewekwa tar.: March 13th, 2020

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa. Mhe Selemani Jafo amewataka watumishi wa Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kujenga mahusiano mazuri mahala pa kazi ili kuweza kutoa huduma bora kwa wananchi.

Ameyasema hayo leo  wakati akifungua Mkutano wa Baraza la Wafanyakazi la Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa  unaofanyika  katika  ukumbi wa Chuo cha Kilimo cha Sokoine Mkoani Morogoro.

Mhe. Jafo amesema Baraza la wafanyakazi linajukumu la  kupitia mipango  ya maendeleo lakini  linapaswa kujadili kwa kina masuala ya mahusiano kwenye  maeneo ya kazi  kwa kuwa majukumu hayawezi kufanyika vizuri bila kuwa na mahusiano mazuri sehemu ya kazi.

“Hatuwezi kutimiza majukumu yetu bila kuwa na mahusiano mazuri, mahusiano ni jambo  nyeti, na la msingi  mahala pa kazi kwa kuwa  Maeneo ambayo hakuna mahusiano bora ufanisi nao hushuka hivyo ni wajibu wa kila mmoja  kuhakikisha tunajenga mahusiano bora kwenye utendaji kazi ”Amesisitiza Mhe Jafo.

Amefafanua kuwa haipendezi kuona Mkuu wa Idara anakuwa kama mungu mtu na kuwanyanyasa watumishi walioko chini yake , jambo hili linashusha ari ya watumishi na kupunguza ufanisi katika utendaji kazi wenye mafanikio.

“Ni wajibu wa Mkuu wa Idara au kitengo kuhakikisha anawapa nafasi watumshi anaowaongoza kutoa maoni ya maboresho ili  kuleta mabadiliko kwenye utendaji kazi wa kila siku, jambo hili litasaidia kuongeza kasi ya kujitoa katika kutoa huduma bora kwa wananachi.” Amesema  Mhe. Jafo

Mhe. Jafo amewataka watumishi kujenga mahusiano  baina ya mtu na mtu, idara na Idara ili kuleta mabadiliko ambayo yatasaidia katika kuweka mikakati imara ya kutoa huduma bora kwa wananchi.

Ameendelea kufafanua kuwa kazi hawezi kufanyika vizuri kama hakutakuwa na  upendo na kuheshimiana miongoni mwa watumishi, hivyo amewataka watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha wanaimarisha upendo na amani miongoni mwao.

“Tatizo la Viongozi wanaopewa dhamana hupandisha mabega na kujikweza pale wanapopewa dhamana   na kuwaona watumishi wengine hawana maana, hiki kitu sikubaliani nacho kabisa, kwenye uongozi  lazima  usimamie haki  na wajibu  lakini ruhusu mawazo  ya wengine kutoka kwa watumishi walio chini yako ili kuongeza ufanisi katika utendaji kazi “ amesema Mhe. Jafo

Amewaagiza baadhi ya viongozi waliopewa dhamana  kuacha tabia ya kuwagawa watumishi na kutengeneza majungu kwa wengine ili waonekane  wazuri na kufanikisha mambo yao, bali wasimamie haki kwa watumishi wote ili kujenga umoja na mshikamano.  

Amewataka watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa nchini kuhakikisha wanaheshimiana  ili  kuweka mazingira mazuri katika maeneo ya kufanyia kazi

Aidha amewashukuru watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa kuonyesha weledi mkubwa katika kutimiza majukumu yao katika kipindi cha miaka minne na kuleta mabadiliko makubwa katika utendaji katika  kuwahudumia wananchi.

Na. Angela Msimbira MOROGORO


Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Bil 16.4/- zarejesha hadhi ya Shule za Sekondari za Ufundi nchini

    January 22, 2021
  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.