• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App

Jafo Atoa Wito Kusaidia Wanafunzi Wasiojiweza ili Kuinua Elimu

Imewekwa tar.: June 30th, 2018

WAZIRI wa Nchi, Ofisi ya Rais, Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa (TAMISEMI), Mhe. Selemani Jafo, leo amekabidhi msaada wa vifaa vya shule kwa wanafunzi wasiojiweza wa shule ya msingi na sekondari za Kata ya Sejeli kijijini Mbande wilayani Kongwa mkoani Dodoma.

Msaada huo utanufaisha zaidi ya wanafunzi mia tisa ni pamoja na madaftari 9,000, kalamu 4,000, penseli 2,800, vifutio 1,200 na vichongeo 1,200 vyote vikiwa ni msaada kutoka kwa watumishi wa Ofisi ya Rais TAMISEMI Makao makuu kwa lengo la kuunga mkono Programu ya “Nipe kalamu na daftari na mimi nisome” iliyozinduliwa mwezi Februari mwaka huu na Mhe Jafo ili kuwasaida wanafunzi wanaotoka katika familia duni.

Akikabidhi msaada huo katika shule ya sekondari Sejeli Mhe Jafo amesema licha ya kuwa serikali inaendelea kutoa fedha kwa ajili ya kugharamia elimu lakini gharama za vifaa vya shule pamoja na sare za shule zinatakiwa kugharamiwa na wazazi au walezi, hivyo baada ya kuona kuna changamoto ya kipato kwa baadhi ya familia ndio sababu pekee ya kuanzisha Programu hiyo.

“Leo wadau wameamua kurudisha fadhila kwa watoto ambao wazazi ama walezi wao hawana uwezo, hili jambo ni kubwa sana tena ni jambo la Ibada, nina kila sababu ya kuwashukuru na kuwaombea, niwasihi watanzania wote waunge mkono jitihada hizo ili Sera ya Elimu Bila Malipo isaidie kuondoa tofauti kati ya wanaojiweza na wasio jiweza” Alisema Mhe Jafo.

Katika hatua nyingine Mhe. Jafo alipokea msaada wa vifaa kama hivyo kutoka kwa Chama cha Umoja wa Waganga wa Tiba Asilia Tanzania (UWAWATA (T)) waliochangia madaftari elfu mbili, huku walimu wazalendo kutoka chuo kikuu cha Dodoma (UDOM) wakichangia daftari 120, kalamu 115 na penseli 70 pamoja na ahadi ya daftari 4,400 kutoka ofisi ya mkurugenzi wa halmashauri ya wilaya ya Kongwa pamoja na madiwani wa halmashauri hiyo.

Aidha, Waziri Jafo ametoa agizo kwa maafisa wa ofisi yake na halmashauri ya Kongwa katika mwaka ujao wa fedha kujenga walau mabweni mawili ya kuanzia kuondoa adha ya kutembea umbali mrefu kwa baadhi ya wanafunzi wa sekondari ya Sejeli.

Awali Kaimu Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa ambaye pia ni Afisa Elimu Sekondari wilaya ya Kongwa Bwana Nelson Milanzi alisema kuwa wilaya hiyo ina wanafunzi 87,185 wa shule za msingi na sekondari kati ya hao wanafunzi 3,523 sawa na asilimia 4.637 wa shule za msingi wana uhitaji wa vifaa vya shule na kusema kuwa kuanzishwa kwa Programu hiyo kutasaidia kuongeza mahudhurio pamoja ufaulu wa wanafunzi.

Naye Mratibu wa Kitaifa wa Programu ya NIPE DAFTARI NA KALAMU NAMI NISOME, Dkt. Ombeni Msuya amesema wanalengo la kufika nchi nzima lakini pia kuwafundisha wanafunzi suala la uzalendo ili hapo baadaye nao wawasaidie watu wengine wenye mahitaji.

“Tuna lengo la kufika nchi nzima sanjari na kuanzisha kambi maalumu ya kuchangia elimu ili kuwafikia wanafunzi wote wenye uhitaji huu, lakini pia tutakuwa tunatoa elimu ya uzalendo ili vijana wetu waje kuwa wazalendo hapo baadaye ili likitokea jambo kama hili wawe mstari wa mbele kama wanavyofanya wadau wengine”

Akitoa shukrani kwa niaba ya wanafunzi wenzake, Rosemary Chimya mwanafunzi wa kidato cha pili shule ya sekondari Sejeli iliyopo Mbande, mbali na kumshukuru Waziri Jafo kwa kuanzisha programu hiyo lakini aliiomba serikali iwajengee mabweni kwa ajili ya kuwaondolea adha ya kutembea umbali mrefu kwenda shuleni pamoja na kuwaongezea walimu wa sayansi, vitabu na madawati.

Zulfa Mfinanga na Fred Kibano



Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Natoa siku siku 12 mtatue kero za soko la Ndugai na Stendi kuu ya Mabasi- Waziri Jafo

    March 03, 2021
  • Agizo la ujenzi wa vyumba vya madarasa 2257 latekelezwa

    March 02, 2021
  • Waziri Jafo ataka Shilingi Bilioni 245 za Miradi ya Maendeleo zitumike kwa wakati

    March 01, 2021
  • Serikali yalegeza masharti mikopo ya asilimia 10

    February 27, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.