• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

JAFO akerwa na miradi ya elimu Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa

Imewekwa tar.: December 12th, 2019

Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Mhe. Selemani Jafo (Mb) amewaagiza Wakurugenzi wote Nchini  wanaotekeleza miradi wa  kulipa kulingana na  matokeo  (EP4R)  kwa ajili ya ujenzi wa miundombinu ya elimu  kuhakikisha  hadi  kufikia februari 15 mwakani  wanakamilisha miradi hiyo kwa asilimia 100.

Ametoa maagizo hayo leo akati alipokuwa katika ziara ya kikazi ya  kukagua miradi inayotekelezwa na Halmashauri ya Wilaya ya Kongwa Jijini Dodoma.

Mhe. Jafo amewataka Wakurugenzi wote watakaoshindwa kukamilisha miradi  hiyo kwa wakati  kuhakikisha wanaandika barua kwa Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kueleza kushindwa kutimiza majukumu  yao ya kukamilisha miradi hiyo kwa wakati  ifikapo tarehe 20, februari,2020

Amemtaka Naibu Katibu Mkuu anayeshughulikia Elimu Bw. Gerald Mweli kuandaa taarifa  ya  wakurugenzi wote walioshindwa kukamilisha  ujenzi wa miundombinu ya elimu kupitia mradi wa EP4R na kuiwasilisha kwa Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa  Mhe. Jafo ifikapo februari, 20 mwakani.

Mhe. Jafo amefafanua kuwa mara baada ya kupokea taarifa hiyo na kuisoma atatoa mapendekezo kwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dokta John Pombe Magufuli juu ya Wakurugenzi walioshindwa kutimiza wajibu wao.

"Miradi hii tunaijenga mahususi kwa ajili ya kuwasaidia vijana wetu waweze kusoma katika mazingira mazuri, Serikali imetoa pesa ya kutekeleza miradi hii lakini kuna baadhi ya Wakurugenzi wameshindwa kusimamia utekelezaji wake ambapo fedha zimeisha lakini bado miradi haijakamilisha wakati katika maeneo mengine wametumia fedha hiyo hiyo na majengo yamekamilika kwa viwango," amesema Mhe. Jafo.

Amewaagiza Wakuu wa Wilaya wote nchini ambapo Miradi ya EP4R inatakelezwa katika Halmashauri zao kuhakikisha wanawasimamia Wakurugenzi ambao wanalegalega katika kusimamia miradi hiyo ili iweze kukamilika kwa wakati na ifikapo tarehe 20 Februari, 2020 wawasilishe  taarifa kama Mkurugenzi wake ameshindwa kutekeleza majukumu yake

Aidha amewaagiza Wakurugenzi  wote nchini  kuhakikisha wanasimamia  kwa weledi ujenzi wa miundombinu ya elimu  ili kuweza kukamilisha miradi  hiyo kwa wakati.

Akikagua ujenzi wa mabweni na bwalo katika shule ya Sekondari ya Kongwa,Mhe  Jafo amemtaka Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa(TAKUKURU) Wilaya ya Kongwa, Abdullah Urari  kuendelea kuchunguza chanzo cha miradi ya elimu kutokamilika huku fedha zilizotolewa zikiwa zimeisha.

"Sijaridhishwa na utekelezaji wa miradi katika sekta ya elimu,afya mnafanya vizuri,lakini elimu hapana,fedha hizi tulizoleta ndio tumepeleka kwa wenzenu wote,iweje hapa hali iwe tofauti,lazima kuna shida hapa.

Mhe. Jafo amewataka TAKUKURU kuchunguza  kama upande wa manunuzi kuna shida na kama kulikuwa na mianya ya ubadhilifu wa fedha za Serikali  ili wahusika wachukuliwe hatua  kwa kukwamisha  mradi huu.

Kwa upande wake Mkuu wa TAKUKURU wilaya Bw. Abdullah Urari amesema tayari wameshaanza kufanya uchunguzi kuhusu mradi huo kwa maelelezo ya Mkuu wa Wilaya hiyo Deogratius Ndejembi aliyowahi kuyatoa.

"Tulichogundua katika uchunguzi wa awali hapa utaratibu wa manunuzi umekiukwa, “force account” haikufuatwa,walifanya makisio makubwa ya vitu na hivyo kupelekea vifaa  vingi kubaki na vitu vilinunuliwa kwa gharama kubwa," amesema Urari.

Awali akisoma taarifa ya ujenzi,Mkuu wa Shule ya Sekondari ya Kongwa Alex Salum alisema Januari mwaka huu walipokea kiasi cha sh milioni 290 toka wizara ya fedha kwa ajili ya ujenzi wa vyumba viwili vya madarasa,mabweni mawili na bwalo la chakula.

Amesema mpaka sasa zaidi ya sh milioni 200 zimeshatumika ambapo ujenzi bado haujakamilika pamoja na kwamba baadhi ya vifaa vya kumalizia ujenzi huo vipo.

"Kwa sasa hapa ujenzi wa bwalo umefikia asilimia 75,ujenzi wa mabweni asilimia 95 na madarasa umefikia kwa asilimia 95,na matarajio yetu ni kukamilisha ujenzi huu ifikapo januari 15 mwakani,"alisema mkuu huyo.

Aidha katika ziara hiyo mbali na kutembelea ujenzi wa miradi hiyo katika shule ya Sekondari ya Kongwa,pia alikagua ujenzi wa maabara na mabweni katika shule ya Sekondari ya Sejeli na sekondari ya Ibwaga kabla ya kukagua ujenzi wa chumba cha upasuaji na maabara katika Hospitali ya wilaya.

Na. Angela Msimbira OR-TAMISEMI




Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Wakurugenzi watakiwa kujitathimini Ukusanyaji wa Mapato

    January 21, 2021
  • Dodoma wapongezwa, wapewa miezi 5 kukamilisha ujenzi wa barabara

    January 20, 2021
  • Shule ya Msingi Nkuhungu yapewa siku 14 kukarabatiwa

    January 20, 2021
  • Asilimia 10 inavyoibua Wajasiriamali Arusha

    January 19, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.