• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App

Jafo akemea mlundikano wa taka kwenye dampo la Dodoma

Imewekwa tar.: January 17th, 2020

Waziri wa Nchi, OR-TAMISEMI Mhe. Selemani Jafo amekemea hali ya mlundikano wa takataka kwenye madampo ya kisasa yaliyojengwa kwenye baadhi ya Majiji na Manispaa nchini kupitia mradi wa mpango miji ya kimkakati (Tscp).

Waziri Jafo amekemea hali hiyo wakati alipotembelea dampo la Chidaya lilipo Jijini Dodoma na kukuta mlundikano wa taka ambayo zimesababisha hali ya uchafu, inzi na harufu katika eneo hilo la kuhifadhia taka.

“Madampo haya yamejengwa kwa gharama kubwa sana na yana lengo la kuimarisha usafi kwenye miji yetu na kuchataka taka hizo kwa utaalamu wa kisasa kabisa usioleta athari zozote za kimazingira huku yakihakikisha usafi wa eneo la dampo unazingatiwa” alisema Jafo.

Aliongeza kuwa naona mitambo ya kuchakata taka hizi imeegeshwa tu na haifanyi kazi na takataka zimelundikana hapa na taarifa mnazonipa haziniridhishi, sioni sababu yeyote ya msingi inayopelekea uongozi wa dampo hili ushindwe kushindilia hizi taka kila zinapoletwa.

Jafo aliagiza uongozi wa Jiji la Dodoma kuongeza usimamizi katika Dampo hilo ili kazi iweze kufanyika kama inavyotakiwa ili kukamarisha usafi wa Jiji la Dodoma ambapo ndipo Makao Makuu ya Nchi.

Pia Waziri Jafo ametoa wiki mbili kwa uongozi wa Jiji la Dodoma kukamilisha matengenezo ya mitambo yote ambayo inahitilafu ili iweze kuwa sawa na kutumika katika kuchakata na kusindika taka katika Dampo la Chidaya.


“Wakati natembelea madampo mengine nilikuta Manispaa ya Kigoma  mitambo imeegeshwa tu bila kufanya kazi inayotakiwa na niliwaambia kuwa mitambo ile nitaihamishia Dodoma kwenye Dampo hili  lakini kwa hali hii siwezi kuleta ile mitambo rekebisheni hii yenu haraka ili kazi za hapa ziendelee kama inavyotakiwa alisisitiza Waziri Jafo.

Akitoa ufafanuzi katika ziara hiyo Mkurugenzi wa Jiji la Dodoma Godwin Kunambi kuwa kwenye bajeti ya mwaka 2019/20 imetengwa bajeti ya shilingi mil 600 kwa ajili ya uendeshaji wa mitambo na dampo la Chidaya hivyo hakuna upungufu katika fedha za uendeshaji na usimamizi ila changamoto hii iliyotokea ya ubovu uliotokea wa mitambo hii haujakwamishwa na uhaba wa fedha ila ni upatikanaji wa vipuli vya mitambo hiyo.

Naye Kaimu Mkuu wa Idara ya mazingira Ally Mfinanga alisema mitambo hiyo iliharibika mwishoni mwa mwezi Novemba, 2019 na mvua zinazoendelea kunyesha zimesababisha magari ya taka kumwaga taka mwanzoni hapo bila kusambazwa kwa sababu gari la kusambaza haliwezi kufika eneo la taka kutokana na mvua hizi.

Aliongeza kuwa mitambo miwili iliyoharibika tumeshaanza mchakato wa kutengeneza magari hayo na yatatengemaa baada ya muda mfupi na kazi ya kuchakata na kusindikika taka hapa Dampo itaendelea vizuri na kwa ufanisi kama ilivyokuwa kama awali.

Dampo hili la kisasa limejengwa kupitia mradi wa mpango miji mkakati na madampo yenye hadhi hii yamejengwa katika Miji ya Tanga, Arusha, Mbeya, Mwanza, Kigoma pamoja na hapa Dodoma.

Mwisho.


Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Kafanyeni Tohara kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi

    March 04, 2021
  • Uhaba wa Saruji wachelewesha ujenzi wa barabara za Mji wa Serikali

    March 03, 2021
  • Natoa siku siku 12 mtatue kero za soko la Ndugai na Stendi kuu ya Mabasi- Waziri Jafo

    March 03, 2021
  • Agizo la ujenzi wa vyumba vya madarasa 2257 latekelezwa

    March 02, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.