• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya

Halmashauri zatakiwa kusimamia kwa karibu miradi ya ujenzi inayotekelezwa kupitia Force Account

Imewekwa tar.: February 13th, 2019

Na Mathew Kwembe, Morogoro,

Serikali imewataka viongozi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa kuhakikisha kuwa wanasimamia kwa karibu utekelezaji wa ujenzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo ili kuleta matokeo yanayotarajiwa kwa umma.

Wito huo umetolewa leo na Mkurugenzi wa Serikali za Mitaa kutoka Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa Dkt Charles Mhina wakati akizungumza na Maafisa Manunuzi kutoka halmashauri 118 wanaoshiriki mafunzo kuhusu marekebisho ya sheria ya ununuzi wa umma  na kanuni zake na mfumo wa utoaji taarifa za manunuzi (PMIS) yanayofanyika mkoani Morogoro.

Dkt Mhina aliwaambia Maafisa Manunuzi hao kuwa halmashauri haiwezi kutekeleza miradi ya maendeleo kwa kutumia force account bila ya kuwatumia wataalamu wake kwani wana jukumu kubwa la kusimamia na kutoa ushauri wa kitaalamu katika utekelezaji wa mradi.

Aliongeza kuwa kwa mujibu wa mwongozo uliotolewa na serikali karibu kila kamati inayohusika katika utekelezaji mradi iwe kamati ya ujenzi, manunuzi, au mapokezi ya vifaa ni lazima iwe na mtaalamu wa halmashauri.

Hivyo Dkt Mhina alisisitiza kuwa endapo kamati hizo zitatekeleza majukumu yake ipasavyo, mfumo wa force account utakuwa na tija kwa halmashauri kwani utawezesha miradi mingi ya ujenzi kukamilika mapema na kuonyesha thamani halisi ya fedha zilizotumika kwenye ujenzi wa miradi hiyo.

Aliongeza kuwa mfumo wa force account unahitaji uongozi wote wa halmashauri uwajibike kwa pamoja katika utekelezaji wa miradi ambapo pia watawajibika kuhakikisha kuwa ujenzi husika unazingatia vigezo vya ubora ili viendane na thamani halisi ya fedha zilizotolewa.

"Force account lengo lake ni kupunguza gharama za ujenzi, hivyo liability ya ubora inahamia kwa mmiliki ambapo halmashauri kupitia kwa mhandisi wa ujenzi anabeba jukumu la kutoa ushauri wa kitaalamu na kuhakikisha kazi inakuwa bora kwa vigezo vilivyowekwa badala ya jukumu hilo kumtwisha mkandarasi,"alieleza Dkt Mhina.

Alisema mfumo huu ni mzuri kwani mahali ambapo mkandarasi angedai alipwe shilingi milioni mia nane zaidi ya gharama halisi za ujenzi kupitia force account fedha hizo zinaokolewa kwani jukumu la usimamizi na mwajibikaji wa ujenzi ni Mhandisi wa ujenzi wa Halmashauri.

Dkt Mhina aliongeza kuwa hata Ofisi ya Rais TAMISEMI inajenga jengo la ghorofa makao makuu Dodoma kwa kutumia mfumo wa Force Account ambapo ili kupata matokeo yanayotarajiwa, viongozi wote wa wizara akiwemo Waziri wa Nchi wamejipanga kuhakikisha kuwa wanasimamia kwa ukaribu ujenzi wa jengo hilo ili likamilike kwa wakati na ubora unaotakiwa.

" Wakuu wote wa Idara wa Ofisi ya Rais TAMISEMI tumepangiana zamu za kuwa site (eneo la ujenzi) pale Mtumba na tunahakikisha kuwa tunasimamia kamati zote za ujenzi kuanzia ile ya mapokezi ya vifaa, manunuzi, na ya ujenzi ili tuweze kukamilisha ujenzi kwa wakati," alisisitiza.

Kwa mujibu wa Dkt. Mhina, Viongozi wa Halmashauri wanapaswa kujipanga vizuri kutekeleza miradi ya ujenzi wa vituo vya afya, hospitali za wilaya na miradi mingine ya maendeleo inayotekelezwa katika halmashauri zao kwa kuisimamia kwa ukaribu.

Mafunzo ya siku nne ya marekebisho ya sheria ya ununuzi wa umma na kanuni zake yanaendeshwa na Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa kupitia Programu ya Maboresho ya Fedha za Umma Awamu ya V (PFRMP V) kwa kushirikiana na Mamlaka ya Udhibiti wa Ununuzi wa Umma (PPRA).



Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Vikundi 13 Wilayani Kibaha vyanufaika na mikopo ya sh milioni 46

    February 25, 2021
  • Magufuli: Viongozi tatueni kero za wananchi kwa wakati

    February 25, 2021
  • Shilingi Bilioni 3 zakwamua Wanawake, Vijana na Walemavu Geita

    February 25, 2021
  • Vikundi 47 Kondoa vyapewa mikopo ya shilingi milioni 147

    February 24, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.