• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App

Dkt.Gwajima: Simamieni kwa weledi utekelezaji wa miradi ya Global Fund

Imewekwa tar.: August 17th, 2019

Naibu Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa anayeshughulikia afya Dkt. Dorothy Gwajima amewaagiza waratibu wote wa miradi ya Afya chini ya Mfuko wa Dunia wa Kupambana  na Ukimwi, Kifua Kikuu na Malaria kusimamia utekelezaji kwa weledi  ili kuhakikisha walengwa wanapata huduma bora kwa wakati na kuongeza kasi ya kudhibiti magonjwa haya kwa Kinga na Tiba.

Ameyasema hayo leo wakati akifunga kikao kazi  cha kujadili  utekelezaji wa shughuli  za Mfuko wa Dunia  wa Kupambana  na Ukimwi, Kifua Kikuu  na Malaria kilichofanyika katika Ukumbi wa Mikutano wa Chuo cha Mipango , Jijini Dodoma

Amesema kuwa, Vita dhidi ya magonjwa haya itafanikiwa zaidi iwapo kila mmoja atawajibika katika nafasi yake na kuhakikisha shughuli zilizopangwa zinatekelezwa kwa wakati na ufanisi na taarifa husika zinatolewa kwa wakati na ubora.

Dkt. Gwajima amesema, viongozi wote ngazi ya Halmashauri wahusike na utekelezaji wa miradi hii kwa kuwa, siyo suala la wataalamu wa afya pekee bali sekta zote wakiwemo Wakurugenzi wa Halmashauri, Maafisa Mipango wa Halmashauri na Waweka Hazina wa Halmashuari.

Amesisitiza kuwa, katika safari ya kuelekea kwenye nchi ya viwanda na uchumi wa kati, sekta ya afya ni mdau mkubwa kwa kuwa, kadri wananchi wenye uhitaji wanavyopata huduma bora za afya kwa wakati na kadri wanavyoepuka maradhi ndivyo wanavyoongeza kasi ya safari hiyo hivyo, kila anayeshindwa kuongeza kasi ya utekelezaji wa miradi hiyo anapunguza kasi ya safari hiyo na atachukuliwa hatua.

Dkt. Gwajima amezipongeza halmashauri 85 ambazo zimefanya vizuri kwenye utekelezaji wa mradi huo kwa kasi kubwa na amezitumia salaam halmashauri zingine 100 ambazo zimesuasua  kwenye utekelezaji wa miradi hiyo na kuwataka  kuandaa maelezo ya kutosha kwa nini wasihesabiwe kuwa wanakwamisha safari ya nchi kwenda kwenye viwanda na uchumi wa kati kwa kuchelewesha huduma.

 “Nimesikitishwa na Baadhi ya Halmashauri nchini ambazo zina kasi ndogo ya kutekeleza miradi hii na ninachokiona hapa ni uzembe tu ambao itabidi wahusika wawajibike, kwa nini wengine watekeleze kwa wakati na ufanisi wengine wabaki nyuma” Amehoji Dkt. Gwajima

Wakati huohuo, amewaagiza Waganga Wakuu wa Mikoa na Wilaya na Waratibu wote wa Miradi hiyo kuwa, wakumbuke nafasi walizonazo ni kama ibada kwa kuwa, zinahusisha masuala ya uhai na uponyaji hivyo, wasimamie kikamilifu utekelezaji wake na kuwashirikisha viongozi wote na kufanya kazi kwa ushirikiano ili kuunganisha nguvu katika kukabiliana na changamoto za utekelezaji.

Aidha amewahimiza kuwasilisha taarifa za utekelezaji zikiwemo stakabadhi za kukiri mapokezi ya fedha kwa wakati.

Na Angela Msimbira OR-TAMISEMI



Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Uhaba wa Saruji wachelewesha ujenzi wa barabara za Mji wa Serikali

    March 03, 2021
  • Natoa siku siku 12 mtatue kero za soko la Ndugai na Stendi kuu ya Mabasi- Waziri Jafo

    March 03, 2021
  • Agizo la ujenzi wa vyumba vya madarasa 2257 latekelezwa

    March 02, 2021
  • Waziri Jafo ataka Shilingi Bilioni 245 za Miradi ya Maendeleo zitumike kwa wakati

    March 01, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.