• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu
    • SIS Mobile App

Dkt. Gwajima awasha motokwa timu ya afya Halmashauri ya Wilaya ya Maswa

Imewekwa tar.: August 14th, 2020

Naibu Katibu  Mkuu, Ofisi ya Rais TAMISEMI anayeshughulikia afya, Dkt. Dorothy Gwajima amemuagiza Mkurugenzi wa Halmashauri ya Maswa, Dkt. Fredrick Sagamiko  kufanya mabadiliko ya haraka kwa Timu ya Afya ya Wilaya  hiyo kutokana na kutokuwa na utendaji mzuri na kuweka watendaji wapya wenye kasi inayotarajiwa na wananchi.

Agizo hilo amelitoa leo Wilayani Maswa baada ya kufanya ziara katika hospitali ya Wilaya hiyo na kugundua timu ya afya kutotekeleza majukumu yake  kwa ufasaha katika maeneo mengi licha ya kujengewa uwezo na Mkoa mara kadhaa bila kuwa na mabadiliko katika utendaji wao.

Dkt.Gwajima amefanya maamuzi hayo baada ya kuona hali ya utendaji wao katika nafasi zao kama timu ya afya ya msingi hawazitendei haki hivyo ili kutoleta madhara makubwa kwa jamii amemtaka Dkt. Sagamiko kufanya mabadiliko kwa haraka.

Aidha Dkt. Gwajima katika ziara yake amepata kukagua vitengo vyote katika hospitali hiyo na kugundua baadhi ya mapungufu katika vitengo hivyo yakiwemo hali duni ya usafi huku kukiwa na vyoo vilivyojengwa kwenye jengo jipya na badala ya kutumiwa vimefungwa na kugezwa kuwa stoo ya vitabu .

Dkt. Gwajima amesema  kuwa  Serikali  ililenga kuwajali wananchi wake, Vilevile, amekagua huduma ya vipimo vya X-ray na kubaini havitolewi kwa sababu ambazo hazina msingi kwani mashine hiyo ipo na inafanya kazi.

“Naagiza  mara moja vyoo vya nje vifanyiwe usafi na mnitumie picha kabla sijafika Dodoma na hivi vipya mlivyogeuza stoo ya vitabu vianze kutumika ndani ya saa 48”,ameagiza Dkt. Gwajima.

Wakati huo  Dkt. Gwajima amewapa masaa 24 tu huduma za vipimo vya X-ray zirejee hapa na wananchi waanze kupata huduma ya vipimo hivyo.

Pia Dkt. Gwajima amemuagiza Mkurugenzi huyo kuwa maelekezo yote na mapungufu yaliyobainika katika hospitali hiyo yawe yametekelezwa kwa ufasaha na kuwasilisha taarifa  katika Ofisi ya Rais TAMISEMI kwa siku zisizo zidi  14.

Katika hatua nyingine Dkt. Gwajima amemtaka Mkaguzi wa Ndani wa Halmashauri hiyo kukamilisha ndani ya wiki mbili taarifa ya matumizi ya dawa bila maeleezo ya wapi zilitumika ili wahusika waweze kurudisha fedha hizo na kuchukuliwa hatua za kisheria kwa kila atakaye kuwa anahusika katika sakata hilo.

“Mali ya Serikali haitumiwi bila utaratibu na bila taarifa hata siku moja , hivyo ukishindwa kuwajibika na kuanza kuiletea hasara kwa Serikali ambayo imekuajiri ili uipe ushirikiano kujenga Taifa ujue wewe ni wa kuwekwa pembeni tu hakuna namna ingine ili nafasi yako apewe mwingine mwenye kujua thamani ya kuwa mtumishi  mwenye weledi katika kuwajibika na kujali ili mali iliyopo iwanufaishe walio wengi katika Taifa”, amesisitiza Dkt. Gwajima.

Akimalizia Dkt. Gwajima amewapongeza baadhi ya watumishi katika hospitali hiyo wanaofanya majukumu yao kama inavyotakiwa akiwemo Afisa Ustawi wa Jamii Bw. Abakos kwa weledi wake katika kuelimisha jamii katika kupenda kujiunga na Bima za Afya na kupunguza wanaotibiwa kwa misamaha kwa asilimia 50.

Naye Mkurugenzi wa Halmashauri ya Maswa, Dkt. Fredirick Sagamiko amesema kuwa maagizo yote yaliyotolewa yatafanyiwa kazi kwa wakati na pale panapohitaji kuchukua hatua stahiki zitachukuliwa kwani awali kulitokea changamoto  na yeye  akafanya mabadiliko.

“Baada ya miezi mitatu tunatamani urudi kuona utekelezaji wa maagizo uliyotoa leo na ninakuahidi kuwa mabadiliko hayo yataleta matokeo chanya katika utendaji wetu”, amesema Dkt. Sagamiko.

Kwa upande wake Mganga Mkuu wa Mkoa wa Simiyu, Dkt. Festo Dugange amemshukuru Naibu Katibu Mkuu kwa kuwa mwalimu mzuri ambaye amezitambua kazi zao walizofanya kwa weledi na kuwapa mbinu nyingi mpya za kufikia mafanikio ya kuleta ubora katika utendaji wao.

“Naamini kuwa kupitia mbinu hizi tutatekeleza ipasavyo na kufanya mkoa wa Simiyu kuwa kituo cha watu kuja kujifunza utendaji kazi mzuri wenye matokeo kwa wananchi”, ameeleza Dkt. Dugange.

Na. Majid Abdukarim, Maswa





Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Kafanyeni Tohara kupunguza maambukizi ya virusi vya ukimwi

    March 04, 2021
  • Uhaba wa Saruji wachelewesha ujenzi wa barabara za Mji wa Serikali

    March 03, 2021
  • Natoa siku siku 12 mtatue kero za soko la Ndugai na Stendi kuu ya Mabasi- Waziri Jafo

    March 03, 2021
  • Agizo la ujenzi wa vyumba vya madarasa 2257 latekelezwa

    March 02, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.