• Wasiliana nasi |
    • Maswali ya mara kwa mara |
    • Malalamiko |
    • Barua pepe za watumishi |
PO-RALG

Jamhuri ya Muungano wa Tanzania

Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

  • Mwanzo
  • Utawala
  • Kuhusu Sisi
    • Local Government History
    • Kuhusu Wizara
      • Directories
    • Dira na Dhima
    • Majukumu ya Wizara
    • Mkataba wa Huduma kwa mteja
    • Idara
  • Mikoa
    • Arusha
    • Dar es Salaam
    • Dodoma
    • Geita
    • Iringa
    • Kigoma
    • Kilimanjaro
    • Lindi
    • Mbeya
    • Mara
    • Mtwara
    • Mwanza
    • Morogoro
    • Kagera
    • Manyara
    • Katavi
    • Pwani
    • Ruvuma
    • Rukwa
    • Shinyanga
    • Simiyu
    • Songwe
    • Tanga
    • Tabora
    • Njombe
    • Singida
  • Miradi na Programu
    • Tanzania Strategic Cities Project
    • MradiwaUendelezajiwaJiji la Dar es Salaam (DMDP)
    • Programu ya Miji Endeelevu (ULGSP)
    • Mradiwa Fursa na Vikwazo kwa Maendeleo (O &OD)
    • v. Mradi wa Kukabiliana na Mabadiliko ya Tabianchi (Decentralized Climate Finance Project)
    • Programmu ya Maendeleo ya Sekta ya Kilimo (ASDP)
    • Uimarishaji wa Mifumo ya Sekta za Umma (PS3)
    • UNFPA
    • Mradi wa Ujenzi wa Ofisi za Wabunge (MP’s Office)
    • Mradiwa Ukarabati wa Vituo vya kutolea huduma za Afya
    • Primary school Development Plan
    • Secondary school Development Plan
    • Programu ya Usambazaji Maji Vijijini
    • Programu ya kuzisaidia Serikali za Mitaa
    • Mpango wa Uboreshaji wa Mfumo wa Serikali za Mitaa
    • Mradi waujenzi wa Kituo cha Kumbukumbu za Serikali za Mitaa
    • Programu ya Uhamasishaji na Uchambuzi wa Sera
    • Mfuko wa Pamoja wa Afya (Busket Fund)
    • LIC
    • Program (PFMRP)
    • Rural - Urban window
    • Mfumo wa kusajili Wajasiriamali Wadogo
  • Kituo cha Habari
    • Habari
    • Maktaba ya Picha
    • Speech
    • Taarifa kwa vyombo vya habari
    • Machapisho ya Halmashauri
  • Machapisho
    • Taarifa Mbalimbali
    • Taarifa za Mapato
    • Majarida
    • Fomu Mbali mbali
    • Presentations
  • Miongozo
    • Miongozo OR TAMISEMI
    • Miongozo ya mradi wa SEQUIP
  • Vijiji na Miji
  • Nyaraka
    • Nyaraka za Elimu
    • Nyaraka za Afya
    • Fomu

Chandarua Pekee Hakiondoi Malaria – Dkt. Kapologwe

Imewekwa tar.: October 26th, 2020

Na. Fred Kibano, Dodoma

Serikali imetoa wito kwa Wadau wa Sekta ya afya nchini kuhakikisha wanatumia njia mbambali za kukijinga na malaria badala ya kutumia njia moja ya chandarua ambayo pekee haiwezi kuondoa malaria na kufikia malengo ya Taifa katika kutokomeza malaria.

Hayo yamesema na  Mkurugenzi wa Idara ya Afya, Ustawi wa Jamii na Lishe Ofisi ya Rais TAMISEMI Dkt. Ntuli Kapologwe wakati akifungua kikao kazi cha afya chini ya T-MARC Tanzania kwa Wadau wa malaria ambao ni Ofisi ya Rais TAMISEMI, Wizara ya Afya na Ustawi wa Jamii, Jinsia, Wazee na Watoto, T-MARC Tanzania na baadhi ya asasi zilizopo kwenye baadhi ya mikoa Jijini Dodoma leo.

Dkt. Kapologwe amesema Wadau wote waige mfano wa asasi ya T-MARC Tanzania (T-MARC) Shirika lisilo la Kiserikali linalofanya kazi ya kuboresha afya ya jamii na kusaidia maendeleo yao ambao wameweza kutumia njia mbalimbali katika kudhibiti malaria kama vile upulizaji wa madawa ya kuangamiza viluwiluwi vya Mbu Kwenye Mazalia, kuwajengea uwezo jamii katika kupima malaria wapatapo dalili za malaria, kutumia chandarua chenye dawa na njia nyingine.

Amesema kuna tabia ya baadhi ya Wadau kufanya kazi za malaria nchini lakini kazi yao kubwa ni kugawa vyandarua ambavyo haviwezi kuondoa malaria kwa asilimia mia moja.

Aidha,amewataka Waganga Wakuu wa Mikoa ya Shinyanga na Simiyu kuhakikisha halmashauri zao zinazotekeleza mradi wa malaria chini ya program ya T-Marc Tanzania zinaendeleza mradi huo kwenye halmashauri nyingine ambazo hazina mradi huo kwa kutenga fedha kwenye bajeti zao.

“sisi kama Serikali kwa maana ya mikoa na Mamlaka za Serikali za Mitaa tuhakikishe program za kudhibiti malaria zinaingia katika bajeti zetu”, alisema Dkt. Kapologwe.

Awali Bwana Hamid Alway Meneja Mkuu wa Mradi T-MARC Tanzania amesema kama ulivyo Mpango wa Taifa wa kudhibiti malaria wa mwaka 2014 hadi  2020 lengo la T-MARC Tanzania ni kusaidia kupunguza malaria nchini kutoka asilimia 7.3 ya 2017 hadi asilimia 1 ifikapo mwaka 2020 ambapo T-MARC wametoa vyandalua vyenye dawa, kujenga tabia ya kupima malaria, kuboresha utoaji wa huduma za afya kwa  wahudumu wa afya na kuzuia malaria hasa kwa akina mama wajawazito.

Bwana Hamidu Alway amesema maeneo yanayotekeleza mradi huo wa malaria unaoisha mwezi Oktoba, 2020 ni Shinyanga halmashauri za Ushetu na Msalala na halmashauri zote za mkoa Simiyu ambapo kiwango cha maambuzi ya malaria kimepungua.

Kazi nyingine zilizotekelezwa ni kutoa mafunzo kwa Wahudumu wa afya ya Jamii ngazi ya vijiji na mitaa, kutumia vyombo vya habari vya redio na machapisho kuelimisha jamii na kutoa pampu na dawa za kuuwa vijidudu vya malaria kiasi cha lita 2,340.

Naye Stella Kajange Mratibu wa Mradi wa malaria na Wadudu Wadhirifu Ofisi ya Rais TAMISEMI amesema wizara itahakikisha vipaumbele vya mikoa vinatekelezwa na Wadau na sio kujichagulia maeneo ambayo hayana tija kwa mikoa.

Kwa upande wake Dkt. Dismas Charles Mratibu wa Mradi wa Kudhibiti Malaria kutoka wizara ya Afya amesema umwagaji wa dawa kwenye mazalia ya mbu unagharamiwa na Serikali kwa asilimia 100 ikiwa ni pamoja na njia sahihi za kutumia kuangamiza mazalia ya mbu hivyo halmashauri zinapopanga bajeti ziingize bajeti za madawa hayo.  

Bwana John Duttu Mratibu wa malaria halmashauri ya wilaya Ushetu amesema kutokana na mradi wa T-MARC Tanzania amefaidika na mafunzo ya upimaji wa maji juu ya kuangamiza viluwiluwi vya mbu kwenye mazalia, kuwapa mafunzo wahudumu wa afya kwenye vijiji na mitaa wilayani ijapokuwa changamoto inayowakabili ni uhaba wa wahudumu wa afya kutokana na umbali wa kijiji na kijiji.



Matangazo

  • Taarifa ya robo ya pili ya mapato ya Halmashauri, iliyotolewa na Waziri wa Nchi Ofisi ya Rais-TAMISEMI January 21, 2021
  • Orodha ya majina ya matokeo ya kidato cha nne,cha pili na darasa la nne January 18, 2021
  • Orodha ya Wanafunzi waliochaguliwa kujiunga kidato cha kwanza Mwaka 2021 December 18, 2020
  • Michoro ya jengo la Ofisi za Halmashauri za Wilaya May 07, 2020
  • ORODHA YA MAJINA YA WALIMU WALIOPANGWA KWENYE VITUO VYA KAZI NOVEMBA 2020 November 27, 2020
  • Orodha ya Vituo vya Afya na Zahanati vilivyo karabatiwa February 27, 2020
  • Angalia zote

Taarifa Mpya

  • Serikali yalegeza masharti mikopo ya asilimia 10

    February 27, 2021
  • Vikundi 23 Wilayani Busega vimenufaika na mikopo ya asilimia 10

    February 26, 2021
  • Vikundi 366 Wilayani Kilwa vyanufaika na mikopo ya sh bilioni 1.1

    February 26, 2021
  • Waziri Jafo ataka Zimamoto, Skauti wakomeshe majanga ya moto shuleni

    February 26, 2021
  • Angalia zote

Video

Tathmini Matokeo darasa la saba 2020
video zaidi

Viungio vya Haraka

  • Miongozo ya OR TAMISEMI
  • Majarida Yetu
  • Wazo la Waziri
  • Maktaba ya picha
  • Fomu mbalimbali
  • Historia ya taasisi
  • Taarifa kwa Umma
  • Maktaba ya picha
  • TSCP kwa Undani
  • Uendelezaji Jiji la DSM DMDP
  • Uboreshaji wa Miji
  • Decentralised Climate Finance Project
  • O&OD Report
  • CAG Report
  • Habari mpya
  • Mfumo wa Kusajili Wajasiriamali Wadogo

Tovuti Muhimu

  • Mfumo wa kuomba vibali vya kusafiri nje ya nchi ( LIVE)
  • Health System Strengthening Resource Center (HSSRC)
  • Ikulu
  • Utumishi
  • Tovuti kuu ya Serikali
  • Wizara ya Afya
  • Ajira
  • Wizara ya Fedha
  • Baraza la Mitihani Tanzania
  • Tume ya Ajira Tanzania
  • Wizara ya Elimu

Waliotembelea kijiografia

world map hits counter

Ramani ya Eneo

Wasiliana nasi

    Katibu Mkuu Ofisi ya Rais Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

    S.L.P: 1923 Dodoma - Tanzania, Afrika Mashariki

    Simu: + 255 (26) 232 1 234

    Simu ya Mkononi:

    Barua Pepe: ps@tamisemi.go.tz

Mawasiliano Mengine

   

Waliotembelea

Imeanza Kuhesabu kuanzia Tar.27. Julai 2015
click here

    • Sera ya faragha
    • Kanusho
    • Ramani

Copyright ©2018 Tamisemi. All rights reserved.