Vigezo Vya Kuanzisha / Kupandisha Hadhi Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

5.2 Vigezo vya kuanzisha Mamlaka ya Mji Mdogo (TownshipAuthority)

Mamlaka ya Mji Mdogo ni Mamlaka ya Serikali za Mitaa iliyopo kwenye Mamlakaza Wilaya. Mamlaka hizi zinaanzishwa pale ambapo palikuwa ni Kijiji ambachokimeanza kuendelezwa na kuwa na mazingira ya kimji. Waziri mwenye dhamanaya Serikali za Mitaa amepewa madaraka ya kutangaza Kijiji au Vijiji vilivyofikiasifa zilizowekwa kuwa Mamlaka za Miji Midogo.

5.3 Vigezo vinavyotakiwa kuzingatiwa:

 1. Kuwe idadi ya watu wasiopungua elfu kumi (10,000);
 2. Kuwe na huduma za jamii zifuatazo: Shule ya Sekondari, Kituo cha Afyana Mahakama ya Mwanzo;
 3. Kuwe na Soko pamoja na Maduka ya rejareja yasiyopungua matano (5);na
 4. Eneo liwe ni Makao Makuu ya Kata au Tarafa.

5.4 Vigezo vya kuanzisha Halmashauri ya Mji (Town Council)

 1. Kuwe na watu wasiopunga 30,000.
 2. Mji uwe na uwezo wa kujiendesha angalau kwa asilimia 50% ya bajetiyake.
 3. Mji uwe na kiwango cha juu cha utoaji huduma ya hospitali, kuwe nashule ya Sekondari, kuwe na angalau maduka ya rejareja yenye leseniyasiyopungua 50, Kituo cha Polisi na pawe na Makao makuu ya Tarafa.
 4. Eneo liwe ni Makao Makuu ya Kata au Tarafa.

5.5 Vigezo vya kuanzisha Halmashauri ya Manispaa

 1. Kuwe na watu wasiopungua laki moja (100,000)
 2. Asilimia 30% ya wakazi wake wawe katika ajira isiyohusiana na kilimo(Non agricultural Sector)
 3. Kuwe na walau kiwanda kikubwa kimoja (Manufacturing industry)
 4. Kuwe na viwanda kadhaa vya “Processing
 5. Asilimia Sabini (70%) ya matumizi ya Manispaa yatokane na vyanzo vyamapato ya Halmashauri (Own Sources).
 6. Kuwe na Huduma ya Kituo cha Elimu ya Watu Wazima.
 7. Kuwe na Hospitali ya Rufaa na Chuo Kikuu.
 8. Ukumbi wa Mikutano wa Kimataifa;.na kiwe ni Kituo cha Taasisi zaKimataifa (Mult National organization.)

5.6 Vigezo vya kuanzisha Halmashauri ya Jiji

 1. Kuwe idadi ya watu wasiopungua laki tano (500,000);
 2. Kuwa na uwezo wa kujitegemea kwa asilimia tisini na tano (95%) kwamapato yake ya ndani; na
 3. Kuwepo sifa nyingine zaidi ya sifa za kawaida za Manispaa kama vilemaeneo ya kihistoria, maeneo ya utalii; Makao Makuu ya Mkoa; kituo chashughuli za Kimataifa na nyinginezo.

Bonyeza Hapa Kupata Nakala ya PDF

Pages: 1  2                

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.