Vigezo Vya Kuanzisha / Kupandisha Hadhi Mamlaka za Serikali za Mitaa.

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa.

1.0 UTANGULIZI

Mamlaka za Serikali za Mitaa huanzishwa kwa kuzingatia Ibara 145 na 146 ya Katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania. Ibara hizi zinaelekeza kuanzishwa kwa vyombo vya Serikali za Mitaa katika eneo la Mikoa, Wilaya, Mji na Kijiji. Ili kutekeleza matakwa haya, Sheria za Serikali za Mitaa zimeweka masharti, misingi na taratibu za kufuatwa katika kuanzisha Mamlaka za Serikali za Mitaa.

2.0 MASHARTI NA TARATIBU

Utaratibu wa kuanzisha Mamlaka za Serikali za Mitaa ni mapendekezo au maombi ya kuanzisha Mamlaka hizo kupata ridhaa ya wananchi kupitia vikao vilivyowekwa Kisheria katika ngazi zifuatazo:

 1. Vijiji.
 2. Kata (Kamati ya Maendeleo ya Kata - WDC).
 3. Halmashauri (Baraza la Madiwani).
 4. Wilaya (Kamati ya Ushauri ya Wilaya DCC.
 5. Mkoa (Kamati ya Ushauri ya Mkoa - RCC).

3.0 VIGEZO VYA KUZINGATIA KATIKA KUANZISHA MAENEO MAPYA YA UTAWALA NGAZI ZA CHINI ZA SERIKALI ZA MITAA

3.1 Vigezo vya kuanzisha Kitongoji

 1. Kaya zisizopungua 50 .
 2. Kifungu cha 30 cha Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Wilaya) inaelekeza kwamba eneo la Kijiji litagawanywa katika Vitongoji visivyozidi 5 (vitano).
 3. Kitongoji ni eneo la utawala katika Mamlaka za Serikali za Mitaa linalotokana na kugawa eneo la Kijiji au eneo la Mamalaka ya Mji Mdogo katika maeneo ya utawala ili kuweza kumudu usimamizi wa utawala katika eneo la Halmashauri.
 4. Eneo la Kitongoji ni eneo la Jimbo la Uchaguzi la Mwenyekiti wa Kitongoji ambaye huwakilisha Kitongoji katika Halmashauri ya Kijiji. Uongozi katika eneo la Kitongoji upo chini ya Mwenyekiti wa Kitongoji.
 5. kifungu cha 13(3) cha Sheria hiyo hiyo kinaelekeza kwamba eneo la Mamlaka ya Mji Mdogo itagawanywa katika Vitongoji kama Mamlaka hiyo ya Mji Mdogo itakavyoamua.
 6. Masharti na utaratibu wa kugawa.

3.2 Vigezo vya kuanzisha Vijiji

 1. Kuwepo kwa eneo la kutosha kwa ajili ya matumizi ya Wananchi kwa sasana baadaye.
 2. Vitongoji visivyopungua vitano (5);
 3. Idadi ya Kaya zisizopungua 250;
 4. Idadi ya watu wasiozidi 10,000;
 5. Upatikanaji wa huduma za jamii kama vile maduka ya rejarejayasiyopungua matano (5), soko, shule ya msingi, zahanati na kituo kidogocha polisi.

3.3 Vigezo vya kuanzisha Mtaa

 1. Mtaa ni eneo la Mamlaka za Miji (Halmashauri ya Mji, Manispaa, na Jiji)linalotokana na kugawanywa kwa eneo la Kata ya Mjini katika maeneo yautawala ili kurahisisha usimamizi wa shughuli za Utawala, Huduma naMaendeleo. Kwa mujibu wa Sheria ya Serikali za Mitaa (Mamlaka za Miji) Namba 8 ya mwaka 1982 eneo la Mtaa hugawanywa kwa kuzingatia idadiya Kaya au sura ya nchi Kijiografia.
 2. Mtaa huwa na Mwenyekiti wa Mtaa ambaye ndiye Kiongozi na mwakilishiwa Mtaa katika Kamati ya Maendeleo ya Kata.
 3. Idadi ya Kaya ambazo zinapaswa kuwepo katika kila Mtaa ni zisizopunguaKaya 50.

3.4 Vigezo vya kuanzisha Kata

 1. Idadi ya Vijiji vilivyosajiliwa visivyopungua vitano (5);(ii).
 2. Ukubwa wa eneo la usiopungua kilometa za mraba 500,
 3. Idadi ya watu wasiopungua 10,000;
 4. Uwezo wa Halmashauri kumudu gharama za ongezeko la maeneo yaUtawala.

4.0 Vigezo vya kuanzisha Halmashauri za Wilaya

 1. Kuwepo na idadi ya Kaya zinazotakiwa kwa eneo kuwa Halmashauri yaWilaya;
 2. Kuwepo kwa idadi ya watu wanaotakiwa kwa eneo kuweza kutambuliwakuwa Halmashauri ya Wilaya;
 3. Kuwa na eneo la ardhi ya kutosha kuendeleza shughuli za kiuchumi,kijamii na kimaendeleo katika Halmashauri ya Wilaya kiwango;
 4. Kuwepo na mapato yanayotarajiwa kukusanywa kama kodi au tozonyingine zenye kutosheleza utoaji wa huduma muhimu pamoja nauendeshaji wa shughuli za Serikali katika eneo zima la Halmashauri yaWilaya;
 5. Kuwepo kwa huduma za kijamii na kiuchumi, kama vile shule, vituo vyaafya, zahanati, maji, barabara kwa kuzingatia viwango vilivyowekwakitaifa kwa kila sekta husika.

5.0 Vigezo vya kuanzisha Halmashauri za Wilaya

5.1 Vigezo Vya ujumla

 1. Jiografia ambayo inafanya utoaji huduma kwa Wananchi kuwa mgumukwa sababu ya milima, mito, misitu, mabonde au Visiwa.
 2. Kuwepo kwa miundombinu inayohitajika kwa eneo la utawala kuanzishwa.
 3. Kuwepo kwa mtandao wa barabara za uhakika kuunganisha Makao Makuuya eneo la utawala lililoanzishwa na maeneo mengine yenye kuhitajikuhudumiwa na Makao Makuu,
 4. Uwezo wa Serikali wa kuanzisha eneo jipya la utawala.
 5. Utayari wa Wananchi kuchangia uanzishaji wa eneo la utawala.Aidha, ili maeneo hayo yaweze kuanzishwa/ kupandishwa hadhi vimewekwavigezo kwa mujibu wa Sheria ya Mipango Miji Na 8 ya mwaka 2007 (The UrbanPlanning Act No 8 of 2007) Kipengele cha Tano cha Jedwali la Tano (Itemnumber 5 of the Fifth Schedule) kama ifuatavyo:-

Pages: 1  2                

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.