Taratibu za Kupandishwa Vyeo na Mafunzo kwa Watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa

Imetolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu Tawala za Mikoa na Serikali za Mitaa

3.0 Utaratibu wa Mafunzo

3.1 Mkakati wa Mafunzo kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa

 • Kwa mujibu wa Mkakati wa Mafunzo kwa Watumishi wa Serikali za Mitaa uliotolewa na Ofisi ya Waziri Mkuu TAMISEMI waajiri wanapaswa kundaa mpango wa mafunzo ya muda mfupi na mrefu kuwezesha watumshi wao kujengewa uwezo.
 • Hivyo Waajiri wanapaswa kufanya tathmini ya mahitaji ya mafunzo kwa watumishi wao kupitia mfumo wa upimaji kazi wa wazi ili mafunzo atakayopangiwa mtumishi yaweze kuziba pengo la utaalam na stadi za kazi lililoonekana kwa mtumishi kutekeleza majukumu yake.
 • Mtumishi atawekwa kwenye Mpango wa Mafunzo wa mwaka kwa kuwa haiwezekani watumshi wote wakaenda masomoni kwa mara moja.
 • Watumshi wataenda mafunzoni kwa utaratibu ulioidhinishwa na Halmashauri bila kukiuka taratibu zilizotolewa na OR-MUU na Wizara za Kisekta kwa mafunzo yanayohusu utaalam.
 • Mpango ulioidhinishwa na Halmashauri ni muhimu uwe wazi kwa watumishi wote ili Watumishi pamoja na wasimamizi wao wa kazi waweze kupanga vizuri ratiba zao za kazi
 • Waajiri chini ya Mkakati wa Mafunzo kwa watumishi wa Mamlaka za Serikali za Mitaa wanapaswa kutoa kipaumbele zaidi katika mafunzo ya muda mfupi ya kuongeza stadi za kazi.
 • Wizara za kisekta chini ya Mkakati wa Mafunzo zinapaswa kutoa mafunzo yanayohusu masuala ya kitaalam chini ya Sekta zao ili kuwaongezea uwezo wataalam wa Kisekta waliopo katika Halmashauri na Mikoani
 • Mamlaka za serikali za Mitaa hazina budi kuhakikisha kuwa wataalamu wake wanahudhuria mafunzo ya uongozi na kuingizwa kazini yanayotolewa na Chuo cha Serikali za Mitaa, Dodoma
 • Watoaji wa huduma za mafunzo katika Mamlaka za Serikali za Mitaa wataratibiwa na kusimamiwa viwango vya huduma zao na Chuo cha Serikali za Mitaa Dodoma.

3.2 Ruhusa za kwenda mafunzoni:

 • Waajiri wanapaswa kutenga fedha za mafunzo kadri ya mahitaji yatakayobainishwa na kukubaliwa na Halmashauri pale ambapo mpango utakuwa umepungikiwa fedha ni wajibu wa Waajiri na watumishi kutafuta fedha za mafunzo
 • Kabla mtumishi hajaenda mafunzoni atapaswa kupewa ushauri nasaha kuhusu mafunzo anayokwenda kufanya kuhusiana na ukuaji wake katika utumishi wa umma
 • Barua ya ruhusa ambayo atapewa mtumishi kabla ya kwenda mafunzoni inapaswa kujieleza bayana kuhusu masharti ya ruhusa hiyo
 • Pale ambapo mtumishi atalazimika kujigharamia kwa ridhaa ya mwajiri ni vema mwajiri kuwa wazi katika ruhusa atakayoitoa
 • Mtumishi akiwa katika mafunzo ya muda mrefu wakati wa likizo anaweza kurudi kufanya kazi katika kituo chake cha kazi au Mwajiri anaweza kumtaka kuripoti kazini na kuendelea na kazi wakati wa likizo hiyo.
 • Baada ya mtumishi kugharamiwa mafunzo na Halmashauri itamlazimu kuitumikia Halmashauri hiyo kadiri Halmashauri itakavyokuwa imeridhia wakati inatoa ruhusa

3.3 Baada ya mtumishi kurejea kutoka mafunzoni:

 • Mtumishi wa Umma akimaliza mafunzo anatakiwa kuripoti kwa mwajiri kwa kutoa taarifa ya maandishi ikiwa ni pamoja na kuwasilisha matokeo ya kufuzu masomo wakati akisubiri cheti.
 • Mwajiri atapaswa kumpongeza Mtumishi mara tu baada ya kuwasilisha cheti cha masomo na kufanya mchakato wa kumbadillishia kazi iwapo atakuwa na sifa za kubadilishwa kazi hii ni pamoja na mahitaji ya mtumishi mwenye sifa aliyopata mtumishi (Ubadilishwaji wa cheo recategorization utazingatia maelekezo yaliyotolewa na Katibu Mkuu, Utumishi).
 • Mwajiri atapaswa kufanya ufuatiliaji wa karibu wa utendaji wa mtumishi baada ya kuhitimu mafunzo ili kumwezesha kutumia ujuzi /Elimu aliyopata na kubaini upungufu kwa ajili ya ushauri na mafunzo mengine ikibidi.

Pages: 1  2                

INFORMATION
Vigezo vya uanzishaji na upandishaji hadhi wa mamlaka za serikali za mitaa
Taratibu za kupandishwa vyeo na mafunzo kwa watumishi wa MSM
Utaratibu wa Jinsi ya Kushughulikia Malalamiko Serikalini.
Maelezo kuhusu utaratibu wa uhamisho kwa watumishi wa Umma
Majukumu Na kazi za Meya,Madiwani,Wenyeviti wa Vijiji na Vitongoji.
EVENTS
SIGN UP

COUNTER STARTED ON:27th July 2015.